2016, PUMZIKA BABA YANGU MZEE AMERIKA NONGWA ,ASANTE BIMKUBWA KAMWELANGA, MMETANGULIA MBELE NA KUUNGANA NA WENZETU WA MJI WA MZEE NONGWA -KIPINGO WILAYANI MALINYI. MUNGU AWAJALIE HERI USONI PA MUNGU WETU. AMEN

              Mzee Raymund Jr (Amerika) Hassan Nongwa 
                                 1925-Julai 23,2016.

Desemba 2012 nilikuwa naye kwa Christ mass, Benjamin ,Faith na Amisa wakimtania Komredi Amerika Nongwa .Mzazi, babu, Mkwe na mzee kwa umma na jamii yake. Mimi na familia yangu tutamkumbuka sana , tunamuombea sana na daima tunakuomba huko uliko kiroho utuombee, Amin

Benjamin na Mama Faith chini mwembe Boribo wa Mzee Nongwa wakiwa na Bimkubwa Kamwelanga ambaye Mei 2016 alituacha baada ya kupatwa na kiharusi. Mungu amrehemu Mama yetu, atuombe vijana wake. Tunamkumbuka sana kwa mawazo jenzi....Alikuwa timamu sana kimawazo na mashauriano.


Wasaa wa furaha sana kati yetu , tunafurahi na kukushukuru kwa maisha bora,mema na Baba wa kweli kwetu sote, umefanya yote na umetuacha vema sana Mzee Amerika-Raymund Hassan Nongwa

IMENICHUKUA MUDA MREFU SANA KUWEKA BAYANA HAPA YALIYONISONGA KWA MWAKA HUU, LEO NIMEONA SI HAKI KUFIKIA 09-DESEMBA BILA KUWAKUMBUKA WALEZI NA WAZAZI WANGU HAWA. 

MUNGU AWAPE REHEMA NA AMANI WALIPO, TUNAWAOMBA MTUOMBEE WANENU. AMEN.