NDUGU RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI , MH.RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2015-

Ndugu Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-2015-

Uchaguzi wa kihistoria uliowakutanisha watu wenye nasaba kiutendaji..kushoto Ndg.Dkt. Magufuli na Ndg. Lowassa kulia.
Kiapo cha uaminifu kwa WATANZANIA,NADHIRI YA KUILINDA NA KUIHIFADHI KATIBA YETU, vyote vikitolewa na Rais mpya Mh. Dkt. Magufuli mbele ya Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Mahakama TANZANIA.
Ulinzi na usalama wa Nchi ulitizamwa na Amiri Jeshi mpya Mh.Rais Magufuli kupitia Gwaride la Majeshi ya Ulinzi na Usalama huku akisindikizwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange

Hongera kwa KAZI NJEMA, nenda kapumzike Mzee Kikwete, hili lilitendeka mbele ya Simba Mlume pekee Africa Comrade Robert Gabriel Mugabe kushoto kwao..hahahaaaaaaa.
Uso kwa uso na Kasisi Askofu Mkuu Polycarp Cardinal Pengo ;Hivi ndivyo Mh.Rais Dkt Magufli alivyoanza safari ya kuingoza Tanzania siku ya Alhamis ya tarehe 05 Novemba,2015. Mungu ibariki Tanzania.