NI MAGUFULI VS LOWASSA.....HAIKUWAHI KUTOKEA TANGU UHURU KWA WATANZANIA KUINGIA MTEGO WA KUAMUA HATIMA YAO

NI MARA YA KWANZA WATAWALA KUSHINDANA NA WAPINZANI WENYE SURA YA UTAWALA.

WATANZANIA WANA HAMU RAIS MTENDAJI NA MBABE...HIZI NDIZO SIFA AMBAZO CHAMA CHA MAPINDUZI ILIZIBAINI NA KUAMUA KUJA NA JOHN MAGUFULI ILI KUHESHIMU KIU YA WANA CCM WALIOJUA HIVO KUPITIA MGOMBEA WA CHADEMA-UKAWA SASA EDWARD LOWASSA.
MGOMBEA WA CCM-MH. DKT MAGUFULI
       MGOMBEA WA UKAWA-CDM MH. LOWASSA

UKAWA WALIJUA KIU HII YA WATANZANIA NA KWA HESABU ZA WAZI HAWAKUWA NA MGOMBEA MWENYE SURA HIYO KWA REKODI, WALIJUA NI CCM PEKEE NDIYE YENYE MTU MWENYE SIFA HIZI NAYE SI MWINGINE BALI NI EDWARD NGOYAYI LOWASSA.

CCM IKIJUA INAPASWA KUPATA MGOMBEA MWENYE HAIBA NA MATENDO YASIYOASHIRIA LELEMAMA NA UPOLE  ILIJUA INAO WATU WAWILI NDANI YA NYUMBA YAKE ILA NI WAZI MMOJA NI ZAIDI YA MWENZIWE .

CCM IKASEMA MAGUFULI NI ZAIDI YA LOWASSA NA KUMTEUA AIBEBE HAIBA NA MATENDO YAKE YA MIAKA 20  KTK BARAZA LA MAWAZIRI AKAHUKUMIWE NA WATANZANIA IFIKAPO OKTOBA 25,2015

CHADEMA-UKAWA KWA DHATI INAAMINI LOWASSA NI ZAIDI YA MAGUFULI NA NI SILAHA YA KUISHINDA CCM, KWA KAULI MOJA BILA KUPEPESA IMEMPA DHAMANA YA KUPEPERUSHA  UKAWA HUKU AKIHUKUMIWA NA REKODI ZAKE ZA MATENDO NA MAAMUZI SERIKALINI.


                                                                                                 
WATANZANIA WAAMUE NI AMA CCM YA JOHN POMBE MAGUFULI AU CHADEMA-UKAWA YA EDWARD NGOYAYI LOWASSA.

Malinyileo....inajiuliza kwa tafakuri tu.....Ni nani mtunzi wa mtihani huu wa 2015 kwa Watanzania hawa?!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA