Nalazimika kusema kwaheri Mkuu Dr. Uli O. Mbamba,ila naomba iwe ya kuonana......Dr. Mbamba akifunga mkutano na kusisitiza juu ya ushirikiano na uwajibikaji kwa wafanyakazi na menejimenti mpya kuhakikisha UCC inasonga mbele , zaidi .

Nalazimika kusema kwaheri Mkuu  Dr. Uli O. Mbamba,ila naomba iwe ya kuonana...kila la heri katika harakati za kuihuisha UDBS......

“HIZI NI ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI” 1995 Mwamba Benjamin W.Mkapa
 Mkurugenzi Mbamba, kwa kipindi hiki kifupi sana kuwa nasi,kimejibainisha kweli ni kifupi kwa sababu wewe na sisi sote tumekubali mioyoni na rohoni kuwa ni kifupi mno kwetu sote.

Binafsi naamini umefanya kitu kikubwa sana ambacho sote tumelazimika kuamini kwa dhati ya mioyo na nafsi zetu kuwa umehudumu nasi kwa kipindi kifupi sana kinyume na mapenzi yetu kwako.
 Dr.Mbamba kwa wewe kuwa nasi, UMETUFUNDISHA KUWA NA HOFU YA MUNGU. Katika hali hiyo miezi yako 19 inabaki kuwa ni kidogo sana kwetu kulingana na kile ulichokipanda mioyoni mwetu.

“HIZI NI ZAMA ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI” Kweli na wazi imedhihiri UCC ndani ya miezi 19 chini yako.

Taarifa hii imenifanya kuukumbuka wimbo mmoja wa Jazz za Kitanzania uloimbwa huko nyuma kidogo  hata kama Binamu yangu Haule siku hizi amezipa kisogo lakini yeye na Kaka yangu Mtui wanaukumbuka huu wimbo japo nikirejea sehemu tu ya mashairi yake " AKHERA HAKUENDEKI DUNIA HAIKALIKI, TUMEBAKI NA MFADHAIKO" , nimejikuta naukumbuka wimbo huu kila nikiiangalia hii mail ya Bint Marwa, natamani sana kutii neno TUMAINI na ni kwa sababu huko mwanzo wa andiko langu fupi nimekiri bayana kuwa “UMETUFUNDISHA KUWA NA HOFU YA MUNGU.”

Naamini atakufanyia njia ktk mapito yako yote, Utuombee. Amen.

Balozi wa Amani.