ASANTE DKT. JUMA NGASONGWA KWA YOTE ULOTUFANYIA....

AMANI KWENU Watu Wangu Malinyi. Mengi sana yameongelewa kuhusu ubunge na Mbuge mtarajiwa. Ni malumbano ya hoja ingawa na jazba pia imo. Ni jambo jema.
Siku za karibuni Wengi wetu wanaongea kuhusu Dr. Ngasongwa kuwa Mbunge kwa miaka 15. Wengi wanalalamika kuwa Dr hakufanya ya kutosha jimboni kwake. Naomba niseme nanyi DR NGASONGWA amefanya kazi kubwa sana ambayo record yake haitavunjwa miaka ya karibuni. Najua wapo watakaopinga haya lakini nawahakikishia hakuna wa kumfikia kwa miaka mingi sana ijayo nanyi mtaona kwa macho yenu.
Mtakumbuka Dr ameingia kwenye ubunge jimbo likiwa hoi kabisa kiuchumi, kielimu na huduma za jamii. Kwa ufupi sana:
1. Amewezesha ujenzi wa shule za kata nyingi kuliko sehemu nyingi nchini. Sekondari mpaka Biro, Igawa, Ngoheranga! Mngeyapata wapi hayo?
2. Upatikanaji wa fedha za ujenzi wa Daraja la Kilombero. Kujenga daraja hapo ni kama miujiza tu. Uchumi wa Ulanga yote hauendani na thamani ya daraja lenye gharama ya 55 bilioni.
3. Mradi umeme kupitia Mlimba wote tuliona kama uwongo wa kisiasa. Sasa sote tunaona umeme unavyoingia Malinyi. Ni ndoto inayotimia.
4. Mawasiliano ya simu ya Aitel, Voda na Tigo yote yapo Malinyi. Nendeni Merera na Chita ambako hawana hyduma hizo licha ya kuwa na viongozi wakubwa wenye mamlaka.
5. Barabara ya Malinyi Ifakara ipo chini ya Tanroads hivyo kupata matengenezo kila mwaka. Sehemu nyingi barabara ni MBAYA kuliko hii yetu. Tembeeni muone ndiyo mtajua Ulanga iko juu sana.
Kuna mambo mengi mengine yakiwemo kuhamasisha kilimo cha mpunga ambacho leo ni ukombozi kwetu. Mpunga unafanya watu wa Malinyi wawe na maisha mazuri sana kuliko wengi wetu huku Dar. Ndiyo maana wengi wetu tunakuja kulima huko Malinyi ili nasi tunufaike.
Kwetu sisi Dr Ngasongwa ni alama ya mpambanaji aliyeonyesha njia jinsi ya kufanya siasa kwa vitendo.
Ni ombi langu kuwa ninyi wapya mnaokuja muendeleze pale alipoachia Babu badala ya kubeza mambo yanayoonekana kwa macho yetu maangavu. Amka mwana Malinyi tushirikiane tuweze kusonga mbele.