WATANZANIA TUNA NINI MIOYONI MWETU JUU YA ALBINO?

Mauaji ya Albino nchini Tanzania yazidi kuongezeka


Muungwana huyu anaishi kwa machale maana yeye na sheshe tofauti hakuna....Watanzania tunaabika sana kwa maisha ya mkato yalojaa shiriki ambayo Mola ameikataa

 Nchini Tanzania mauaji ya watu walio na ulemavu wa ngozi au Albino yameripotiwa kuzidi kuongezeka. Hii ni baada ya mtu mmoja mwenye ulemavu wa ngozi kuuwawa mkoani Simiyu na baadhi ya sehemu zake za mwili kunyofolewa

 
Huyu mdada hapo yuko na hofu rohoni na mwilini maana hajui amuamini nani asimuamini nani!!!

Mauaji ya Albino yamekuwa yakishirikishwa sana na imani za kishirikina. Watu walio na ulemavu huo wa ngozi sasa wameitaka serikali nchini humo kuwapa ulinzi zaidi. Amina Abubakar alizungumza na Babu Sikare ambaye ni mlemavu wa ngozi anayeishi Dar es Salaam nchini Tanzania, Mwanzo anaelezea hisia zake juu ya mauaji ya hivi karibuni.