RAIS KARUME AHOJI KAMA SIYO LOWASSA NI NANI NDANI YA CCM?

Sioni Tofauti za Kimantiki Kati ya Hotuba ya Mhe. Zitto Kabwe na ile ya Ndg. Lowassa ....... Dk. AMANI ABEID KARUME
Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) yenye makao makuu yake jijini Bonn Ujerumani tulipata wasaa wa kumtembelea mstaafu huyu ili kupata mawili matatu kama mstaafu lakini vile vile kama mwana siasa mkongwe Nchini Tanzania....
MWANDISHI; Mhe. Raisi Mstaafu kwanza pokea salaam zetu lakini pili mzee tukushukuru kwa kutukaribisha na kutupa wasaa wa kutusikiliza ila kwa kweli umekuwa husikiki kabisa Mhe......
KARUME; Karibuni sana lakini pili usihangaike sana kuni adress kwa jina reeeeefu na kwa cheo mwandishi wewe niite tu kwa jina langu Amani ama Abeid au Karume. Halafu hilo la mimi kutosikika ulitaka nisikike wapi? Maadali umekuja mpaka kwangu sasa hapo utanisikia.... Mfiwa ndiye anayelia anafikwa na msiba sasa mimi pia siwezi kusikika hovyo tu kama mwendewazimu ila mnaponitafuta mtanisikia.
MWANDISHI; Mhe. Karume tukushukuru tena sisi tumekutembelea kukusalimu baada ya kutokukusikia kwa muda mrefu lakini si vibaya vile vile ukituruhusu tuweze kuulizana mambo machache hasa katika swala zima la kisiasa na maoni yako juu ya Taifa letu hili.
MHE. KARUME; Ahsanteni kwa salaam ila nyie waandishi mi nawafahamu barabara hizo salaam mimi naamini si hoja hata kidogo hoja ya msingi ni hiyo ya pili haya endeleeni nawasikiliza.....
MWANDISHI; Mhe. Karume ni miaka kadhaa sasa imepita toka kustaafu kwako na tunaamini ni mengi mema utakuwa unayashuhudia na vile vile kuna changamoto kadhaa utakuwa unaziona, nini hasa mtazamo wako kuhusu haya yote....
MHE. KARUME; Unajua kuna mambo mengine unaweza kujibu yakazua tafrani na hasa ukizingatia namna ambavyo ninyi mnaripoti ila yatosha kusema hivi kila zama na ngoma yake ndugu waandishi..... Na kila ngoma huchezwa kwa staili yake hivyo zama zangu ngoma iliyokuepo tuliicheza na sasa aliyepo naye anacheza ngoma yake na naamini Ndugu zangu wa Zanzibar nikiwemo mie tunaridhishwa na namna ambayo Zanzibar inaongozwa. Changamoto hazikosekani manake anayeongoza si Malaika ila kubwa bado sote tunabaki kusimama kama Wazanzibar tukiwa wamoja na tukiwa tumeshikamana ili kulinda heshima na historia ya wale waliotufikisha hapa tulipo.
MWANDISHI; Mhe. Karume wewe Muundo huu ww Serikali kwako unauo naje??
MHE. KARUME; Kwanza swali kama hili mara nyingi huwa sipendi kulijibu na bahati nzuri sikuwahi kuulizwa na hata kama nimeulizwa sikuwahi kulijibu kwa undani ila niseme tu kwa ufupi Muundo wa Serikali yetu si kwa manufaa ya Karume ama Shein la hasha! Ni kwa maslahi mapana ya watu wa Zanzibar sasa kama Wazanzibari wameafiki na kupendezwa na hili mimi ni nani nipaze sauti yangu kinyume na matakwa ya Wazanzibar?
MWANDISHI; Sasa Mhe. Karume una maana kwamba una unga mkono muundo huu?
MHE. KARUME; Naunga mkono kile walichokiamu na walichokubaliana Wazanzabari kiwe.
MWANDISHI; Mhe. Karume kuna baadhi wa watu wamepata kusikika wakisema umekuwa hutoi ushirikiano kwa Serikali hii iliyopo hivi sasa kuna ukweli wowote juu ya maneno haya?
MHE. KARUME; (Kicheko) Sasa hili unataka nikujibu je? Manake umesema kuna maneno ila ungeniambia Raisi kasema angalau ningefikiri mara mbili...... Ila kwa kuwa si Raisi alhamdulilahi..... Umekuja leo kwangu sasa hayo maneno hayana maana tena.... Kama nilivyokueleza awali Karume nitafutwapo nipo na niitwapo wito nauitika.
MWANDISHI; Swala la Muungano Mhe. Karume kwa upande wako mpaka sasa limekaa je!
MHE. KARUME; Kwangu swala la Muungano limekaa vile vile kama ambavyo Watanzania wanaliona... Sina jambo jipya sana ila Watanzania wajue Muungano wetu huu hauna mfano na kimsingi Muungano huu ndio hasa unaitufanya tuzidi kumwona Marehemu Mzee Karume na Marehemu Mzee Nyerere. Tuendelee kuuenzi na kuutetea manake nje wa Muungano sote sisi hatupo.
MWANDISHI; Mhe. Karume Taifa sasa lina mambo makubwa mawili ama matatu ambayo yako mbele Katiba na Uchaguzi wewe una lipi la kusema? Tukianza na Katiba...
MHE. KARUME; Nianze na Katiba kwanza nilitaka kukuambia mambo ya ngoswe yabaki kwa ngoswe ila kama Mtanzania niseme hivi kimsingi mimi sioni kama tuna haja na kukimbizana na hii Katiba kwa speed kubwa namna hii unless tunataka kuweka rekodi Duniani kwa kuwa Nchi ya kwanza kutengeneza Katiba kwa muda mfupi.
Lakini vile vile tunaweka hiyo Rekodi hivyo ili iwe nini?? Tunasikia matatizo ya BVR hivi kweli mpaka kufikia tarehe 30.04 tutakuwa tumeandikishwa wote?
Katiba ni jambo jema ila ni lazma kama Watanzania tushauriane na kukubaliana kwamba jambo hili halihitaji haraka wala ulazimishwaji. Twendeni pole pole ili tufike salama. Manake hii yaweza kuwa balaa ama laana kwa Taifa kama tusipokuwa makini...
Swala la uchaguzi si mara ya kwanza sisi kufanya uchaguzi hivyo naamini chaguzi zitakwenda salama na Inshallah atapatikana mwingine wa kuendesha kurudumu hili.
MWANDISHI; Mhe. Karume tunapoelekea huko kwenye uchaguzi wewe ukiwa kama mwana CCM nafasi ya ndugu zenu Wapinzani unaio naje?
MHE. KARUME; Unafahamu bwana miaka hii nilianza kuona kama Wapinzania wanaweza kuwa kwenye nafasi kubwa na kuleta Changamoto ila ghafla tena nashangaa kuona wenzetu hawa wakitoka kabisa katika misingi ya umoja, misingi ya demokrasi na kuendekeza misingi ya migawanyiko ambayo lazma itapelekea kuwabomoa.
MWANDISHI; Mhe. Karume ni nini hasa msingi wa hoja yako?
MHE. KARUME; Wewe mwandishi na hata Watanzania wengi mlianza kuona nguvu ambayo Chama kama CUF au CHADEMA iliyokuwa nayo lakini kumbe ndani yao bado wamejawa ubinafsi, chuki na kuoneana.
Hivi ni nani aliyewahi kufikiri ingefikia mahali mtu kama Zitto angefukuzwa ndani ya hicho Chama lakini leo pamoja na kazi njema aliyofanya kukijenga Chama, kutumikia Taifa lake kama Mwenyekiti katika Kamati nyeti bado kafukuzwa kwa mambo ya kusadikika.
Mimi niseme hotuba ya yule kijana binafsi iliniuma sana ni hotuba nzito iliyosheheni ujumbe mzito na yenye uwingi wa busara. Manake ni kweli kwamba lile usilopenda kutendewa usimtendee mwenzio haifai hata kidogo. Wewe leo unampiga mawe Karume kesho unaenda Hospitali unamkuta Karume ndo anapaswa kukufanyia upasuaji... Unaweza kufa hata kabla ya kuingia chumba cha upasuaji na kitakacho kuua utakuwa ni ugonjwa wa wasi wasi na mashaka.
Hotuba ya Zitto binafsi ilinikumbusha sana hotuba ya Bwana Edward Ngoyai Lowassa alipokuwa akijiuzulu uzito wa maneno yake hayatofautiani na haya ya Zitto. Lowassa alisema tatizo ni Uwaziri Mkuu lakini aliongeza vile vile kwamba wote mle Bungeni ni wanasiasa sasa wangeanza kunyoosheana vidole asingepona hata mmoja. Hotuba za namna hii si mchezo ni hotuba nzito na yenye maana sana. Ila ndiko tulikofikia kama Taifa wale wenye nia njema ya kusimamia maendeleo wanaonekana kuwa vikwazo hivyo hutafutiwa mbinu za kuwaondoa.
MWANDISHI; Mhe. Karume umegusia swala la Lowassa nadhani umeona yanayoendelea ndani ya chama chenu na baadhi ya adhabu zilizotolewa... Wewe lako ni lipi juu ya hayo ukizingati wewe ni mmoja kati ya wale wazee wa Baraza....
MHE. KARUME; Usitake kunikorofisha ba bwana wakubwa hawa niseme tu pale tutakapohitaji kusema haya ndani ya vikao vya Chama tutakwenda kusema. Chama hiki kina utaratibu watu hawapaswi kuonewa wala kubezwa. Watu watanunua bidhaa inayouzika sokoni na siyo inayolazimishiwa mteja. Watanzania hawa wanajua wanamtaka nani hata muwazuie kwa kuta za majabali ikifikia mahali uvumilivu na uzalendo wao utawashinda na tutaliweka Taifa hili pabaya.... Watu waachwe waoneshe hisia zao kadri wanavyofokewa na kutishiwa ndivyo nao watakapoendelea kufanya.
MWANDISHI; Mhe. Karume amesikika msemaji wa Chama akizungumzia swala la watu kwenda kushawishi mtu kwamba ni kinyume cha taratibu za chama na muhusika anaweza akaenguliwa kugombea....
MHE. KARUME; Wewe sikiliza huyu mtendaji hana tofauti na Tundu Lissu wewe hukumu imetoka umekimbia kukutana na waandishi bila kukaa vikao vinavyohusika. Zamani sisi ndani ya chama ukisikia Msemaji wa Chama akikutana na waandishi wa habari atakachoanza kusema ni hivi..... " Kikao flani (CC, NEC etc) kilichoketi tarehe chini ya Mwenyekiti wake flani kimeazimia yafuatayo.........."
Huu ndo utaratibu sasa anapotokea mtu na kutamka yake basi hayo yanakuwa yake si ya Chama. Ndani ya CCM huo utaratibu haupo hata kidogo....
Na nashangaa Viongozi nao wamekaa kimya huku ni kukiua Chama. Watafurahia leo kashambuliwa flani ila hawawezi jua kwamba kesho yaweza kuwa ni wao..... Mambo kama haya lazma yakemewe.....
MWANDISHI; Swali la mwisho la kizushi watu wanasema una urafiki wa karibu na mmoja wa wale wanaotajwa kugombea Urais.. Hili limekaa je Mhe. Karume
MHE. KARUME; Mimi nina urafiki wa karibu sana na Bwana Lowassa hilo wala si la kuficha na labda huyo ndiye anayesemwa. Tena nataka niseme hivi kwa hapa siasa za Nchi yetu tulipofikia ningekuwa na uwezo ningemwigta Lowassa nimwombe aachane kabisa na shughuli hiyo. Lakini wakati mwingine mke wangu ananiuliza sasa Lowassa asigombee ili agombee nani?? Na hapo ndipo ninapokosa majibu kabisa. Tunaishia kujipa majibu wenyewe kwamba kwa sasa hakuna mwenye uwezo alio nao Lowassa.....
MWANDISHI; Sisi tukushukuru sana Mhe. Karume kwa ushirikiano wako... Tunakuomba usituchoke pale tutakapokusumbua tena.... Ahsante sana Mhe.....
MHE. KARUME; Ahsanteni na Karibuni sana na msiondoke bila kupataa ka[truncated by WhatsApp]