NI ZITTO HUYUHUYU NDIE KIONGOZI MKUU WA ACT aka MAO WA ACT TANZANIA?

KIFAHAMU CHAMA KIPYA CHA KISIASA CHA ACT-TANZANIA NA MALENGO YAKE, JE KUVIFUNIKA VYAMA VYA UPINZANI VILIVYOPO KWA SERA ZAKE KABAMBE ?, MFAHAMU MAO WAO MPYA NA MWENYEKITI WAKE MWANZILISHI. 

CHAMA kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimeanzishwa na kupewa usajili wa muda huku kikitamba kuwa mbadala wa vyama vyote vilivyopo sasa kwa maelezo kuwa vimekosa demokrasia ya kweli.
Miongoni mwa viongozi wa muda wa chama hicho ni Samson Mwigamba ambaye sasa ndie Katibu Mkuu wa ACT alitimuliwa uanachama wa Chadema kutokana na kuhusishwa na waraka uliotaka kumwandaa Zitto Kabwe kuwania uenyekiti wa chama hicho.

Mao wa ACT  Zitto Kabwe akiwa na Mshauri wake mkuu Prof Kitila Mkumbo wa UDSM kushoto.
Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, alitimuliwa pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo, huku uanachama wa Zitto aliyevuliwa nyadhifa zake zote zikiwamo za Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni,ulikoma ndani ya CHADEMA baada ya kushindwa kesi  mahakamani.
 Mao wa ACT Tanzania Zitto  Kabwe akiweka wazi uanachama wake wa ACT wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Wazalendo kupitia ACT chini ya uongozi Mao wao Zitto wakiimba kwa utii wimbo wa Taifa letu Tanzania.