MALINYI NA SIASA ZA KIBUNGE MMOJA AJA MWENYEWE WAWILI WATUMA WAWAKILISHI.....TUJIPIME SASA.. NI SAHIHI KUWAPISHA VIJANA ?...

Vijana wasomi wenye asili ya bonde la Ulanga Kilombero....wakijiongeza ktk vyuo mbalimbali Tanzania

Wapendwa Wana Malinyi, tunawasalimu.
Tunapenda kuwajulisha kuwa jana Jumapili tarehe 29 March tulifanya mkutano wetu wa Wana Malinyi na Ulanga Magharibi kama tulivyopanga awali. Mambo mengi yalijadiliwa lakini ya muhimu kuyasema kwa watu wote ni suala la Wilaya Mpya na suala la Wana Ulanga ambao WAKATI UKIFIKA WANGEPENDA KUTANGAZA NIA.
Kuhusu wilaya lilikuwa ni suala la kupashana habari juu ya kinachoendelea kwenye mchakato. Mengi yanaendelea lakini jambo la msingi ni kuwa TUSUBIRI MAAMUZI RASMI YA SERIKALI.
Kuhusu na suala la kutangaza nia za UBUNGE wakati ukifika tulipata Wana Ulanga 4. Watatu walikuwa ni Wawakilishi na mmoja alihudhuria mwenyewe kama ifutavyo:
1. Michael Sigaliye alimuwakilisha bwana Simon Ngonyani. Kwa mujibu wa Sigaliye, Ngonyani anaunga mkono Wagombea vijana. Kwa sasa Nganyani hategemei kutangaza nia lakini kama MZEE atatangaza nia yeye naye atatangaza nia.
2. Rayna Wigila alimuwakilisha Hidaya Usanga. Kwa mujibu wa Wigila, Hidaya Usanga anategemea kutangaza nia muda ukifika.
3. Ndegemwema alimuwakilisha Vicent Tira. Kwa mujibu wa Ndegemwema, Bwana Vicent Tira anategemea kutangaza nia muda ukifika.


Kijana Mwanasiasa na Msomi Antipas Mgungusi jana aliitikia wito wa kukutanishwa na watia NIA wenzake hapa Dar . Uamuzi wake wa kuja yeye mwenyewe na kuacha mambo yote yanayomuhusu  ilimpa nafasi ya kujieleza kwa baadhi ya wana Malinyi waishio Dar es salaam.
4. Bwana Antipas Mgungusi alihudhuria yeye mwenyewe na hivyo aliujulisha mkutano kuwa wakati ukifika atatangaza nia.
Hivyo mpaka sasa tumepokea watia nia wanne ambao ni jukumu la wana Malinyi kuwapima na kumchagua mmoja anayefaa ZAIDI.
Tuliruhusu MTIA NIA pekee aliyekuja mwenyewe ajieleze na aulizwe maswali na kwa kuepusha kupokea  majibu yasiyo rasmi ya MTIA NIA aliye nje ya mkutano kutoka kwa Wawakalishi wao waliopo ktk mkutano kwa mfano Bi Khidaya aliwakilishwa na Ndg.Wigira wa Sofi pia MC Doza..na Ndg.Tira alimtuma ndg.Ndegemwema ambao wao walitupa ujumbe wao na sisi kuwaruhusu wakae maana kimsingi tulipoteza sifa ya kuwahoji, hii kwa mujibu wa hekima za wahenga "MJUMBE HAUAWI"

MALINYI OYEEEEEEEE