Kinana amuonya Nape kuhusu Lowassa! Ataka Lowassa aachwe, asisakamwe!


Mh.Lowassa akifurahi na Katibu Mkuu Ndg Kinana jimboni Monduli  pembezoni ni Muenezi wa CCM Taifa akijitafakurisha....
Sasa ni kazi kwenda mbele..Kinana na Lowassa wakikagua miradi ndani ya Monduli...Wanabodi,

Kama nilivyopokea Nape Nnauye Ashambulia Waandishi wa Habari.

Wakati ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana Ikiendelea Mkoani Arusha na ikionekana kuwa na mafanikio makubwa hali ya sitofahamu imeonekana kujitokeza kati ya Nape Nnauye na waandishi wa habari anaoongozana nao katika msafara huo.

Hali hiyo imejitokeza jana wakati wa mapumziko katika Wilaya ya NgoroNgoro. Kinachosemekana kuwa chanzo cha tatizo ni habari zilizoripotiwa na Gazeti la Mwananchi juzi zilizobeba kichwa cha habari "Lowassa Safi, Nyalandu Anazurura.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka Ngorongoro vingi vikiwa waandishi wenyewe wanasema Nape hakupendezwa kabisa na habari hizo zilizoripotiwa na gazeti la Mwananchi na hivyo kutaka kujua ni nani aliyeandika hizo habari na ni nani aliyemtuma.

Waandishi wengi walibaki kushangaa na wengine walifikia hatua ya kutaka kuachana na ziara hiyo wengi wakiona kama wanadhalilishwa wao na tasnia yao........ Wengi walijiuliza wamekuwa wakiripoti yote yanayotokoa kama ambavyo wanavyoyashuhudia na hawakuwahi kutukanwa namna hiyo.... Je tatizo ni habari ama Lowassa?

Nape alionekana kumtuhumu Lowassa kuwa ndiye aliyeshinikiza waandishi waandike hivyo.... Swala hili lilimfanya Katibu Mkuu aingilie kati na kumtaka Nape afute kauli yake na asithubutu kumuhusisha Lowassa kwenye maswala ya kipuuzi tena ukizingatia kazi nzuri na maandalizi mazuri yaliyofanyika katika Wilaya yake.

"Wewe Nape embu sikiliza kwanza usitake kuvuruga msafara huu kwa kutaka waandishi waandike unayoyataka wewe dont do that........ This people quoted me and not you....... Na ni kipi ambacho sikusema kwa mujibu wa gazeti la mwananchi? They are very right.....

Jambo la pili Nape nilishawahi kukuambia na narudia tena leo usipende kumuhusisha ama kumwingiza au hata kumtaja Edward kwenye mambo ya kudhani....... Edward has nothing to do with all this........ Bado unaendelea kukua jitahidi kuwa mwepesi kujifunza sana na maneno ya kutumia uwe unayapia..... Edward atoe hela ili iweje no! no tumemaliza kazi Jimboni kwake tumwache sasa tutaonekana watu wa hovyo sote.

Kinana alimalizia kwa kuwataka radhi waandishi wa habari na kuwaomba wachukulie mambo hayo kama Changamoto kwako na kwa Chama pia.

Waandishi walionekana kukubaliana na busara za Katibu Mkuu na wakamwomba waongee faragha...... Japo hatujapata yaliyojiri katika kikao hicho cha faragha ila inasemekana kuwa kubwa lilikuwa ni kumwomba Katibu Mkuu azungumze na Nape na amkanye asithubutu tena kuwatamkia maneno ya hovyo na yasiyo na heshima kwao.

Na habari zilizotufikia hivi punde msafara wa Katibu Mkuu umepata ajali na kuna baadhi ya watu walioumia kidogo akiwemo Mbunge wa Viti maalumu Catherine Magige. Waandishi wamesikika wakisema yote hayo ni nuksi za Nape Nnauye.

Ziara ya Ndgu Kinana inaendelea leo wanatoka NgoroNgoro kwenda Karatu.

  PASCAL MAYALA'S Take.
Hii Kauli ya Kinana kumtaka Nape asimsakame Lowassa is not good at all!. Inaashiria Kinana ameishaijua hatma ya Lowassa ndani ya CCM hivyo anamtaka Nape aepuke 'adding an insult to an injury', siku zote nasema humu, "I fear the Greeks especially when they bring gifts". Kwa ajili ya aibu wengi hupenda ku stub from the back, lakini Giriki lina ku stub infront while smilling!

Hivi ndivyo ninavyomuona Kinana!. Ukiisha jua siku ya majinjo itakuja, Huna tena sababu ya kupiga makelele, nitachinja, nitachinja!, tulia tuu siku ya mchinjo watu wachinje tuu!. Huku kupiga piga makelele kwa Nape kunaweza kupelekea siku ya kuchinjwa ataonekana alionewa kwa sababu Nape aliisha onyesha dalili za kichinjo!

Source ya hii habari ni Michuzi.
Pasco

Msimamo wetu:
Malinyi Leo inashikilia msimamo wake kuwa CCM inamuhitaji Lowassa na Lowassa anaihitaji CCM.

Kila hila na ghiriba ya kutenganisha CCM na Wana CCM ni kuizika CCM.