ITEETE, SOFI, MALINYI, IGAWA, NGOHERANGA NA KILOSA KWA MPEPO UNGANENI TUPATE WILAYA MPYA KWA MIPAKA MIPYA


 Acheni nongwa zenu niwape wilaya ninyi wapogoro....Mh. Rais Dkt. Jakaya M.Kikwete

Kiona mbali wa ukweli Mheshimiwa Waziri wa zamani Viwanda na Biashara Alhaj Dkt. Juma Ngasongwa aliyeasisi agenda ya Wilaya mpya 2005-10, hapo akiwa na Rais wa Awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa ndani viwanja vya sababa katika maonyesho ya Sabasaba 2003

SALAAM TOKA MALINYI LEO
RCC Mkoa wa Morogoro imeazimia kuigawa wilaya ya sasa ya Ulanga na kuzalisha wilaya mpya katika sehemu ya eneo la Jimbo la Uchaguzi Kibunge la Ulanga Magharib panapo majaaliwa Julai 2015.
Zoezi hili lilikuwa likamilike mwaka wa fedha wa 2014-15 kama siyo uasi uliofanywa na Mbunge wa sasa Ndg Dkt.Mponda.
Ilikuwa ni azma ya serikali ya CCM 2005-10 kuigawa Ulanga lakini azma hii iliingiliwa na mihemuko ya siasa za kijimbo.
Mwaka 2010 -11-13 kwa nyakati tofauti wananchi wa Ulanga Magharib wamekuwa wakipaza sauti kuidai wilaya mpya ya Malinyi.
Mwaka jana kwa makusudi Kanseli ya Ulanga ilitengua maamuzi ya awali ya kutaka wilaya katika mipaka ya jimbo baada ya kushindwa kuridhiana nadani timu ya madiwani wa CCM na pia hata wale wan je ya CCM. Umma wetu nao ulijikuta ukishabikia kulinda mipaka ya zamani bila kuzingatia hoja mpya zilizoletwa na wale waliotaka mipaka mipya. Kanseli iliajiri Mshauri Elekezi ili atoe muongozo kwa mizania ilosheheni weredi wa utawala na serikali za mitaa. Mshauri elekezi alishauri njia ya mipaka mipya ndio iipasayo Kanseli ya Ulanga katika kuzaa wilaya mpya ya Malinyi.
Hoja hii ikasogea Mkoani hapo ndipo Mbunge wetu akaanzisha maandamano ya wahuni kuja Lupiro kwa mapikipiki toka Mtimbira  ili kujenga mazingira ya kumuaminisha Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuwa umma wetu hautaki mipaka ya sasa ibadilishwe…tulipojibidisha kutaka kujua nini msukomo nyuma ya maandamo na upinzani wa Mbunge tuliridhika kuwa alifanya hayo si kwa ajili ya uzalendo bali ubinafsi ili kulinda Ubunge wake lakini pia kutafuta fursa ya kuhamisha wazo zima la makao makuu ya wilaya toka Malinyi na kuisogeza Mtimbira ambako yeye anaamini ni eneo rafiki kwake binafsi kisiasa na uasili.
Malinyi Development Concern iliijibu fitina hii ya Dokta Mponda kwa barua aliyoandikiwa Mh. Rais na nakala zake kwenda Mh. Waziri mkuu, Waziri wa Nchi Tamisemi..Mkuu wa Mkoa na Madiwani wetu wakiwemo wabunge wote wa Ulanga . Tulilazimika kuandika barua hii baada ya ziara ya Waziri Mh. Ghasia aloifanya kwa ghafla baada tu Bunge la Bajeti la 2014-15. Tuliguswa pia na kauli ya Rais aloitamka Lupiro pale aliposema yeye hana nongwa ila kwanza tukubaliane wenyewe kwa wenyewe kwanza.
Jana Ijumaa wana Ulanga wamefikiwa na ujumbe wenye maagizo ya RCC ambao umeazimia kuanzisha Wilaya mpya katika kile tunachokiamini kuwa dhamira safi ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Watanzania kuwa anatekeleza ahadi yake ya 2005/2008/2010/2013 pale alipotua kwa mara kwanza ya pili na tatu ndani ya jimboni Ulanga Magharibi.
Timu hii ya mkoa imeonyeshwa mipaka ya zamani na ile inayopendekezwa lakini pia wamelazimika kujua utayari wa miji ya Malinyi na Mtimbira katika kuwakarimu wateule watarajiwa wa Rais kimakazi na mazingira ya kiutendaji.

Kazi hii imekamilika jana Malinyi baada ya kuanzia Mtimbira.
Ninachowaomba ndugu zangu haitoshi kuridhishwa na ujio tu wa timu hii sambamba na ukaguzi wao…Ninashauri viongozi wa vyama, dini ,jamii kuhimiza wananchi kuwa mipaka mipya mdio mpango unaotakiwa.
Tuwe wakweli toka moyoni na tujitokeze kwa viongozi wa mitaa,Udiwani na vyama vya siasa ,makasisi wa imani mbalimbali waunganisheni wananchi katika kuidai wilaya kwa mipaka mipya.
Hata kama Tume hii si ya kisiasa ila inahitaji kusikia yowe na kilio chetu…hatutaki watu wapigane bali sasa wakati umefika” TUVUNJE UKIMYA-WILAYA MPYA KWA MIPAKA MIPYA”

Wananchi wa Malinyi,Igawa,Ngoheranga,Biro,Sofi na Kilosa kwa Mpepo….hatutapewa tunachostahili ktk kusubiri au kuamini tu kuwa hawa watalaam watatupa haki yetu …Tusikae kimya..tumewaonyesha uwezo wetu kimazingira,Makazi,Miundombinu na huduma za jamii lakini ninawaambia kwa mtu aliyedhamiria kutudhulumu hataishia hapo.
Achaneni na wanasiasa mufilisi waliojaa uoga ktk kusimamia mambo yanayogusa maslahi mapana ya Umma wetu,si agenda ya Kisiasa na kambi zake ,siyo wasaa wa kutenganishwa ili tushindwe…NI WAKATI WA KUHESHIMU MANENO YA WAHENGA WETU- UMOJA NI NGUVU. Basi lile la Umoja ni Nguvu ni rejea sahihi ya jinsi wazazi wetu walivokuwa ktk kuamini kwa umoja wao. Tusiyumbe wana Malinyi.
PIGA KELELEEEEEEE…..TUWAAMBIE CCM NA WATAWALA NI MALINYI KWA MIPAKA MIPYA.
****Malinyi tafuteni kwanza Ufalme wa Mbinguni na mengine mtaongezewa****