BURIAN MHESHIMIWA KAMISAA COMRADE KAPTEN JOHN DAMIANO KOMBA-1954-2015

http://pamojapure.blogspot.com/2015/03/mazishi-ya-kapteni-komba-yafanyika.html#.VPbPZyw8TIVhttps://www.hulkshare.com/millard_ayo_/claudia-john-komba-mtoto-wa-9-wa-marehemu-komba
Rais JAKAYA KIKWETE na mkewe Mama salma Kikwete sambamba na viongozi mbali mbali wa kitaifa wanawaongoza mamia ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni JOHN KOMBA katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwili wake umepokelewa kwa heshima huku ukiwa umebebwa na Askari wa bunge huku ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao huyo aliyefariki duniani katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam hapo juzi.

Katika salamu zake kwaniaba ya kambi Rasmi ya upinzani Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh.Joshua Nasari ametoa pole kwa marehemu na taifa na kusema kamba kambi rasmi kuwa kambi ya upinzani imeguswa na kifo cha mwanasiasa mwenzao kwani kila mmoja atarejea na huko ndiko kila mmoja atakwenda kwa hivyo yatupasa kutengeneza mazingira mazuri kwa familia kwani hakuna ajuaye siku yake ya mwisho ya kufa.

Amesema katika kipindi hiki kigumu nidhahiri kwamba kila mmoja anapaswa kusali na kuomba kwani wao kama kambi rasmi ya upinzani imekuwa nisehemu ya kuweka siasa mbali na hivyo kuungana na taifa na familia katika kipindi hiki kigumu.


 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mh. Saidi Mtanda akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Kamati yake.
 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kushoto) akitafakari na marais wastaafu akiwemo Rais wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto), Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa

Hivi ndivyo Dar es Salaam ilivomuaga Kapten John Komba....Mwana CCM kindakindaki,Msanii,Mbunge na Mwanajeshi Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge wa Mbinga Magharib na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaamtarehe 28.Februari 2015  saa kumi jioni.

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1954 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.


 Kilichotokea ni timilizo la Mwenyezi Mungu ambaye katika maandiko yake alisema, "Bwana alitoa, na Bwana ametwaa" (Ayubu. 1:21).

Mwenyezi Mungu alitupatia mtihani katika maisha yetu na kutukumbusha hatima ya jasho letu aliposema, “Kwa jasho la uso utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe ni mavumbi na mavumbini wewe utarudi” (Mwanzo 3:19).

“Say: ‘It is God Who gives you life, then gives you death; then He will gather you together for the Day of Judgement about which there is no doubt’: but most men do not understand. To God belongs the dominion of the heavens and the earth, and the Day that the Hour of Judgment is established.” (Qur'an 45: 26-27)
Malinyi leo tunaungana na Watanzania wote ktk kuomboleza kifo cha kiongozi, na mtu shupavu aliyetumia talanta yake kwa ustawi wa Tanzania.

Pumzika kwa Amani Kapten John Damiano Komba