BURIANI DADA YANGU MPENDWA ROSELINA AMELIKA RAYMOND NONGWA....07 OKTOBA 1972----08 NOVEMBA 2014

Bi ROSELINA AMELIKA RAYMOND HASSAN NONGWA (RIP) 07-10-1972-08-11-2014

Roselina au Rose Nongwa ni jina maarufu miongoni mwa familia yetu ya Nongwa, Malinyi na Dar es Salaam.

Bi Rose Nongwa amefariki dunia tarehe 08 Novemba 2014 ktk hospital ya Lugala Malinyi Ulanga na kuzikwa jumanne ya tarehe 11 Novemba 2014 katika makaburi ya Njale-pale Soko mjinga-Kipingo Malinyi.

Rose Nongwa amepoteza uhai baada ya kusumbuliwa na maadhara fungus kwenye  ubongo wake ambayo yalidhihiri mwaka 2012 na kupatiwa matibabu katika hospital za Madona Tabata,Amana Ilala na hatimaye Lugala Malinyi Ulanga.

Marehemu Rose amefariki akiwa ni mjasiliamali anayejihusisha na umiliki wa duka la dawa Baridi; hii ni baada ya kupata mafunzo ya msingi ya Uuguzi msaidizi mwanzoni mwa miaka ya 90.

Ni mhitimu wa elimu ya Sekondari aliyoipatia Mtwara Technical Secondary scho kati ya 1988-1991.

Rose Nongwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa kwa mama yake bi Mwanaharusi Maria Kamwelanga na ni mtoto wa tatu toka mwisho kwa mzee Amelika Raymond Hassan Nongwa. Marehemu Rose hajaacha watoto na hakuwahi kuolewa.

Tunawashukuru sana matabibu wote na viongozi wa kiroho kwa kila huduma iliyofanyika mpaka umauti wake. Wana Malinyi wote tunawshukuru na kwa dhati namshukuru sana Bi Sunniva Kilibaha kwa kuwa karibu na Rose mpaka siku ya mwisho ya maisha yake hapa duniani.

Kama familia tulifanya tulichoweza na kufunuliwa na Mungu lakini ni dhahiri hatukufanya 100/100....mbele yako dada yangu tusamehe kwenye mapungufu yetu na utuombee salama mpaka siku tutakapoonana.

Mungu Twakuomba umpe raha ya Milele na apumzike kwa Amani. Amina.

Norbert.A.R.H Nongwa