HEKAHEKA MALINYI YA MACHI 2014 KATIKA PICHA.........

Hapa ni Mto Kilombero mahala ambapo Ujenzi wa Daraja unaendelea na hii ni Ferry ya kuwavusha wana Ulanga Kilombero kwenda na kurudi NYUMBANI

Mafuriko yaliyoikumba Malinyi wiki iliyopita na hii ndio main Road kwenda Lugala Lutheran Hospital-Mjini Malinyi. Hapa ni maeneo ya Kangumba

Naaam suala si mafuriko tu bali na uduni wa Miundo mbinu yetu tokeaa Ruaha-Ifakara-Kivukoni -Lupirro -Malinyi-Ngoheranga -Songea; barabara hii ya TANROADs haijapata huduma makini takribani miaka minne sasa, pichani wananchi wakiitangulia gari maeneo ya Msitu na Mbiga na Livambanjuki; taarifa zinasema kuna daraja Iragua limengolewa na mafuriko....barabara ikiwa iko hoi bila matengenezo makini; hili ni eneo kati ya Tarafa  ya Lupiro-Iragua-Itete kuja Tarafa ya Mtimbira.