Leo asubuhi, ofisi ya serikali kijiji cha Mngeta Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro imefungwa na wananchi wa kijiji hicho na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji hicho kujeruhiwa vibaya kwa kipigo kufuatia madai ya wananchi ya ubadhirifu na uzembe uanaofanywa na serikali yao.

Hatua hii imekuja wiki moja tu kufuatia ile ya kijiji cha Chita kufanyiwa hivohivo.

Akiongea na mwana JF aliyeko kijijini hapo, mwenyekiti wa kijiji hicho aliyekimbilia mafichoni bwana Matei Mwamhanga, amekiri kutokea kwa hali hiyo kijijini hapa na kwamba wananchi wamejichukulia hatua mkononi kufuatia malalamiko ya muda mrefu.

Mengi ya malalamiko hayo hasa lile la kupatiwa umeme ni ile ahadi ililotolewa na Mbunge Abuu Mteketa ambaye hajawahi kukanyaga eneo hilo tokea atoe ahadi hiyo wakati wa kuomba kura.

Wananchi wa Chita na Mngeta wamekasirishwa zaidi na kitendo cha Shirika la Tanesco kuanzisha mradi wa kuweka nguzo za umeme toka Kihansi na kuzichepusha kupeleka Mahenge kupitia Chita huku wakiiacha Chita na Mngeta ikiwa haina huduma hiyo.

Mpango wa kupeleka umeme Mahenge unatokana na nguvu ya kiutendaji ya Mbunge wa Mahenge Mama Selina Kombani, huku udhaifu wa Mbunge Mteketa wa Jimbo La Kilombero ukivikosesha vijiji hivyo huduma hiyo wakati umeme huo huanzia kwenye Wilaya ya vijiji hivyo.

Kesho wananchi wa Chita na Mngeta wameapa kuandamana hadi Kihansi ili kudai haki yao ya kupatiwa umeme na kuwa hawataruhusu umeme upelekwe Mahenge mpaka vijiji vyao vipatiwe umeme kwanza!!!

Mwana JF aliyeko katika msafara huo wa kwenda Kihansi atazidi kuwapasha kinachotoke!!