WANAWAKE NA NDOA; WATUMISHI WAANDAMIZI WANAVYOVUNJA NDOA ZA RAIA

http://freebongo.blogspot.com/2013/08/aibu-mke-afumaniwa-akigawa-uroda.html
 Timbwili I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita  na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao..

Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.

Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.


Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.


 Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.

Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo .

 Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.

Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.

 Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.


Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia.
 

Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.

Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.


Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
 


Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.

Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.


Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.

“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.

Source: Global publisher


 
Afisa wa Serikali yetu  Dkt. Mtarajiwa Rwekaza akiwa amefumaniwa na mke wa Samora
Hiki kisa hapo juu ni cha kweli na siyo uzushi.
Malinyileo tuna ushauri wa bure ktk hulka hii ovu.......

Mwanamke huyu msomi Bi Khadija bila haya wala hofu ya Mungu anamsaliti mumewe tena kwa kumleta Rwekaza nyumbani kwake yeye na Mumewe Samora eti kwa sababu Samora hayupo nyumbani....hii ni laana na chukizo kwa Mungu. Lakini kama mwanamke msomi, je huyu anapaswa kuhudumu UDSM? jibu ni hapana maana hafai kwa lolote kijamii. Tujiulize ni kiwango gani cha dharau huyu mwanamke anakionyesha kwa mume wake? Ni njaa gani ya ngono iliyomfikisha kufanya ufisadi huu? Ni utumwa gani wa fedha, sifa, fursa ambavyo alivitaraji kwa Rwekaza? Kama Samora angeliua  jamii ingelimuhukumje? Kwa kudhihiri kwa ufisadi huu wa Khadija na kuumizwa huku kwa Samora jamii inataka nini toka kwa Samora? Ni nini matunda ya udhariri wa Khadija? 

Wanawake na Wanaume mliooana kwa hiari yenu , kumbukeni sur zenu za siku ya agano kabla ya kudharirisha agano lenu, picha za siku ya ndoa zenu zinaonyesha historia yenu, huenda leo unasifiwa umzuri sana...basi angalia picha zako za ndoa na uchumba na ujiulize huyu niliye naye alipenda nini wakati huo na kwa nini huyu Kibopa/Boss/Kiongozi leo ananitaka na kunisifia mie mzuri sana? Jasiri haachi asili na siyo kila king'aacho ni dhahabu; Uzuri wa leo mama ni msingi wa Mumeo kuchakaa hata kama unaona leo unajiweza kimapambo na mengi mengineyo kimaisha kiasi sasa unaamini kweli wewe ni mzuri. Ni kweli wewe ni mzuri Bi Khadija na ndio msingi wa Samora ktk ujana wako na wake aliamua kuwaacha wote kwa ajili yako......Je Khadija unazikumbuka picha za urafiki wako na Samora? Ni wewe yuleyule au sasa uko mpya? Majibu ni hapana.

Mtumishi mwandamizi wa Ofisi ya Rais utumishi wa Umma-Chuo cha Magogoni Rwekaza akivunja ndoa ya ndugu Samora ambaye yasemekana ni mtumishi wa UDSM kwa udhaifu na unyonge wa mkewe bi  Hadija ambaye naye yasemekana ni mtumishi wa UDSM. Rwekaza ni Mtumishi wa Idara nyeti kwa nchi yetu na kwa unyeti huu amepewa fursa ya kufundisha vijana wetu pale chuo cha Utumishi wa umma Magogoni. Je huyu huyu anastahili kuhudumu katika ofisi za Serikali yetu? Hapana ndio jibu sahihi. Si Rwekaza tu wako wengi wa namna hii ktk safu za kusaidia uongozi wa hapa nchini, wanatumia misamaha ya kodi, suti za bure,mafuta ya bure na safari nyingi nje kama wasaidizi wa wakuu wetu wana mchezo huu mchafu. Rais Obama alimfukuza mkuu wake wa Makachero ingawa tunaaminishwa Jenerali yule alijiuzuru eti kulinda heshima! Thubutu yake, ni Obama huyu huyu aliyewafukuza Makacherowake walioenda Columbia kujihusisha na makahaba; America ilikaribia kumtimua Rais Clinton kwa hulka ovu za kikware akitumia ulevi wa madaraka....Kuna Senator alijitoa kugombea uteuzi baada ya kubainika ukware wake...Wenzetu wako wakali kwa watu wasio waaminifu kwenye ndoa zao. Jamii yetu iamke na kusema sasa hapana. Pamoja tunaweza.

 Pole sana Samora kwa yote yalokupata, sisi hatuna haki ya kukuamulia lakini Mungu akupe njia na hekima juu ya hili. Samora na Khadija wasingelifikia hapa kama si uhalifu/ufisadi/ubazazi wa Rwekaza; Ujumbe wetu kwa wana ndoa wote daima unabaki"Ndoa na iheshimiwe"
Malinyileo