OFISI ZA TRA INAPOGEUKA KUWA MAHABUSU YA WATEJA WA BIDHAA.                                                      TUZIBE UFA LEO.
 Tanzania Revenue Authority
                              OFISI ZA TRA INAPOGEUKA KUWA MAHABUSU
                                             YA WATEJA WA  BIDHAA.


“mambo ya masoko ni muhimu sana na haipaswi kumuachia mkuu wa masoko pekee” kauli hii ya jeff Faulkner inanijia akilini kila ninapotaka kulijadili suala lolote muhimu kwa familia au jamii. Faulkner anatufundisha kuwa kwenye mambo muhimu yanayoiendesha jamii hatupaswi kujiweka pembeni na kuachia wengine. Masoko ndo roho yakampuni kwa maana ndo hukuza au kuua kampuni husika hivyo kampuni nzima inapaswa kuweka nguvu zake hapo na wala si kumuachia mtu au kikundi cha watu. Asante Faulkner kwa fundisho hili.
Ninapoitazama kwa macho yangu ya kuzaliwa TRA naiona maana halisi ya kauli ya Faulkner. Ni taasisi muhimu ni roho ya serikali, roho ya taifa. Ninapoitazama kwa macho yangu ya kuzaliwa TRA naiona maana halisi ya kauli ya Faulkner. Ni tasisi muhimu ni roho ya serikali, roho ya taifa au kwa  wale wasiopenda Kiswahili sanifu wataiita “jembe” la serikali. Hapa ndipo maendeleo yetu yalipo kama taifa.
Taasisi hii inapaswa kupendwa na kuungwa mkono na kila mmoja wetu. Watu wanatakiwa waiamin na kuikubali kwa dhati ya moyo. Uzalendo wetu uanzie hapa kwa kuulinda moyo wa serikali na taifa kwa kuupenda na kuupa ushirikiano. Tuwe na dhamira ya kweli ya ujenzi wa Taifa kwa kuipa ushirikiano TRA na wala sio kuiachia mzigo huu peke yake maana inafanya kazi muhimu kweli. Ifike siku tuseme sisi sote ni TRA moyoni na hapo tutakuwa tumefanikiwa kwa kweli.
Pamoja na ukweli niliouelzea hapo juu wa kuipa ushirikiano tasisi hii lakini bado TRA wenyewe wanajukumu kubwa la kutushawishi kuipenda, kuiamini na mwisho kuipa ushirikiano wa kutosha ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa urahisi ili kufikia malengo iliyojiwekea katika ukasanyaji wa kodi. Maana najua peke yao hawataweza kama alivyisema bwana Faulkner. TRA inawepaswa kutushawishi kuiunga mkono kwa kutuonyesha  inafanya kazi katika ukweli na uwazi na sio kufanya mazingaombwe katika kukusanya kodi.
Sababu hasa za kuandika haya leo kuamsha wahusika juu ya utaratibu ambayo sidhani ka upo kisheria unaotumiwa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA na polisi katika kukusanya kodi. Utaratibu huu nitakao ueleza hapo chini umekua kero kubwa kwa wananchi wengi na wafanyabiashara hasa wa eneo la kariakoo. Na naomba niweke wazi mimi pia ni mmoja wa wahanga wa mchezo huu ambao binafsi naamini ni mchafu hasa kwa yale niliyoyaona na kuyasikia.
Sasa naomba niulezee mchezo wenyewe ambao bado nasisitiza una kila dalili za kuwa mchezo mchafu. Baadhi ya wafanyakazi wa TRA wa tawi la Shaurimoyo wakishirikiana na polisi wamekua wakikamata bidhaa za wateja wanaotoka madukani eneo la kariakoo na kisha kukagua stakabadhi za wateja hao.Baada ya ukaguzi na wao wanapohisi stakabadhi ina tatizo humwambia mteja waende ofisi za Mamlaka ya Mapato zilizopo mtaa wa Shaurimoyo. Hapa ndo nina mashaka napo.
Anapofika ofisi mteja hunyang’wa funguo ya gari au kukabidi mizigo hiyo kwa walinzi na stakabadhi zake huchuliwa na kisha huambiwa asubiri mpaka mfanyabiashara aliyemuuzia aje ndipo aweze kuachiwa kuendelea na safari. Hii sidhani kama inatofauti sana na mtu kuwekwa sero katika kituo cha polisi.
Anapowekwa sero hiyo ya TRA mteja huyo atakaa hapo nje akipigwa na jua akisubiriwa huruma ya mfanyabiashara aliyemuuzia godoro aliyepigiwa simu na TRA aje ili aweze kuachiwa. Hapo mteja atamaliza masaa akisubiri huku akipigwa na jua pengine kuanzia saa 4 asubuh mapka saa 7 ndo mfanyabiashara atajitokeza na kwenda kwa afisa wa TRA.
Kuja kwa mfanyabiashara huyo pekee hakutoshi kumfanya mteja wake kuachiwa na TRA hata kama mzigo huo hauna makosa yoyote mpaka atakapo lipa hela inayotiwa ndo mteja ataachiwa aende zake. Hivi ndivyo TRA yetu inavyokusanya kodi kwa kuweka wananchi mahubusu  tena juani kwa makosa ambayo mengi wao hawahusiki nayo kabisa.
Naomba niweke wazi kabisa binafsi nauona mfumo kama uliokaa kimazingaombwe tu na una kila dalili za rushwa ndani yake. Nasaema hayo kwa kuwa naamini kabisaa kwa akili ya kawaida kabisa huwezi kushikilia mizigo ya mteja ambayo ni imenunuliwa kwa  njia halali na huku mteja akiwa na stakabadhi halali eti kwasababu muuzaji wa bidhaa anadaiwa na TRA tena madeni ambayo hayuhusu kabisa mizigo iliyokamatwa.
Jambo lingine ambalo nalo linaniondoa shaka juu ya imani yangu kwamba mchezo huu ni kuwa pamoja nakuona wafanyabiashara wakiingia na fedha ndani lakin wengi wao walitoka bila stakabadhi yoyote kuonyesha kwamba kuna malipo yaliyofanyika kihalali. Kuna mwingine nilimsikia akimwambia mwenzie atume hela hiyo kwa huyo mfanyakazi kupitia moja ya mitandao ya simu.

Sikatai TRA kukusanya kodi lakini sikubalia kabisa na mfumo huu wa kuwatesa wananchi kwenye jua kali na kuwasababishia usumbufu mkubwa. Natambua ukweli kwamba TRA wanauwezo mkubwa wa kuwapata wafanyabiashara wadanganyifu kwa kutumia njia nyingine nzuri na si hii ya kuwasurubu wananchi. Na kama huu sio mfumo rasmi wa kukusanya mapato wa TRA basi sasa inapaswa kuhakikisha mchezo huu mchafu unadhibitiwa ili kuondoa kero inazozileta.
TRA itambue kabisa kwamba kwa kuendekeza michezo michafu ya aina hii itaondoa imani yake kwa wananchi na wafanyabiashara na hivyo kuiachia peke yake suala la kukusanya kodi. Wahusika wanapaswa kulitambua hili sasa na kuziba ufa huu kwa kuwa licha ya kusababisha usumbufu kwa wananchi lakini pia inakosesha serikali maana unatoa mwanya kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wasio waaminifu kupeana rushwa kutokana na ukweli kuwa wafanyabiashara wengi hawajui sheria au wanaogopa usumbufu wa vyombo vyetu vya usalama.
Huo ndio ufa wetu wa leo ni matumaini yangu shughuli za kuuziba zitaanza sasa na wala sio kesho ili kuwapa imani wananchi na wadau wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini kwa kutambua ukweli swali la kukusanya kodi ni letu sote na wala hatuwezi kuiachia TRA pekee kuifanya kazi hii kama nilivyoeleza hapo juu.
        Imeandikwa na Mlembele Yusuph wa SAUT- Mwanza.