CCBRT-TUNAWAPONGEZA SANA KWA KUWAJALI WANA MALINYI-ULANGA NA WATANZANIA KWA UJUMLA

Nahonga Changala wa Stephan Njitango(Ayu nahonga wa Malinyi leo) akisubiri matibabu ya macho hapa CCBRT-Msasani Dar es Salaam.Wagonjwa wa macho toka Malinyi Mama Bint Mbombwe wa Tuunge kushoto na Mama Bint Kiponda wakiwa wodini CCBRT-Msasani jana nilipowatembelea.
Mama bint Kisenime na baadhi ya wamama kina Bint Makolela wa Biro wakiwa wodini CCBRT.
.
Nahonga Bint Changala wa Njitango akiongea na Mdau wa karibu wa Malinyi leo ndg.Syriacus Chali pamoja na mjomba Tuunge ndani ya wodi ya macho CCBRT
Wagonjwa wa macho na maumbile toka trafani Malinyi -Ngoheranga wakiwa wodini CCBRT.

Malinyi leo jana ilitembelea CCBRT baada ya kupata taarifa ya ufadhiri wa huduma ya macho na maumbile kwa jamii yetu ya Malinyi kupitia shirika hili la hiari.

Picha zilizoonekana ni za wadogo zetu,dada zetu, mama zetu, baba zetu na akina bibi ama babu walioletwa na CCBRT hapa Dar es Salaam usiku wa Jpili toka Malinyi.

Huduma ya utabibu inaendelea vema na kwakweli hawa ndg zetu wako kwenye mikono salama na yenye huruma ya kweli.

Malinyi leo inachukua fursa hii kuwashukuru Serikali ya Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Watumishi na viongozi wote wa CCBRT kwa moyo wao wa kizalendo wanaouonyesha kwa wana Malinyi hawa na waTanzania kwa ujumla.