SIMBA SPORT CLUB NDANI BUTIAMA....USO KWA USO NA MAMA MARIA NYERERE

Mama Maria Nyerere amekuwa mwenyeji wa viongozi na wachezaji wa klabu ya soka, Simba Sports Club kijijini Butiama.Wana SSC na Basi lao ndani ya Butiama kwa Mwalimu Nyerere.Wachezaji wa Simba Sport Club wakitafakari kwa kina mahala alipozikwa wa Baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Simba Sports Club wakaribishwa Butiama na Mama Maria Nyerere

Mama Maria Nyerere wiki hii amekuwa mwenyeji wa viongozi na wachezaji wa klabu ya soka, Simba Sports Club kijijini Butiama.
 Wageni hao wamepita Butiama wakielekea Musoma ambako  wanacheza mechi ya kirafiki.

 Baadhi ya viongozi walioongozana nao ni kocha mkuu Abdallah Kibadeni na kocha wa walinda mlango (ambaye alikuwa mwanafunzi mwenzangu Shule ya Sekondari Tambaza) James Kisaka.

 Wageni walipata fursa ya kuzuru kaburi la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye amezikwa Butiama.


  
Picha: Kaburi la Mtemi Nyerere Burito (kushoto), na la mke wake wa tano Mgaya wa Nyang'ombe (kulia). Nyumba ya mviringo ndipo ilipokuwa nyumba ya Mtemi Nyerere 

Picha: Sanamu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Mwitongo, sehemu alipozaliwa. 
 
Picha: Nyumba iliyojengwa kuzungukia kaburi la Mwalimu Nyerere, eneo la Mwitongo, Butiama.

Habari kwa hisani ya :

Ujumbe toka Muhunda aka Madaraka Nyerere