KONGAMANO LA AMANI, HAKI ITAWALE KULINDA AMANI

http://www.wavuti.com/4/post/2013/07/raiskikwete-afunga-kongamano-la-kujadili-amani-ya-taifa.html#axzz2aWEiooBg Akitoa mada kuhusu mchango wa vyombo vya dola katika kudumisha amani au kuharibu amani kwenye kongamano la mustakabali wa amani na usalama wa taifa kwa miaka 50 ijayo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, mhadhiri wa shule ya sheria ya chuo hicho bwana Onesmo Kyauke amesema matukio hayo yamejitokeza kutokana na jeshi la polisi kuzuia maandamano kwa kigezo cha uvunjifu wa amani, wakati wa sheria za nchi zinaainisha kuwa maandamano ni haki ya kisheria.

Akitoa mada kuhusu mchango wa siasa na dini katika kudumisha au kuharibu amani,mhadhiri wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadetha Killian tatizo lililopo nchni ni serikali kutimia zaidi njia ya kudhibiti migogoro badala ya kutatua hali iliyosababisha viongozi wa vyama vya upinzani kukamatwa na kuachiwa kila wakati ambapo ameshauri kuundwa kwa chombo chakushughulikia migogoro.
Kwa upande wake mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika shule ya habari Dokta Ayub Rioba kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha amani na usalama, amewataka waandishi wa habari kuchagua maoni yakuandika katika kipindi cha migogoro na kutoa fursa kwa pande zote mbili zisikike kwa namna inayosaidia jamii kuelewa na kusaidia mgogoro kutatuliwa.
Akifunga kongamano hilo, waziri wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi amesema serikali imekuwa ikichukua hatua za kinidhamu kwa jeshi la polisi ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya askari 102  na maafisa 6 wa jeshi  hilo wamefukuzwa kazi na kesi zao ziko katika mahakama ya kijeshi ambapo kuhusu maandao amesisitiza swala la kufuata sheria.