RAHA YA MILELE IWE JUU YAKO NA UMPUMZIKE KWA AMANI MAMA MPENZI SAINA AGNES HUSSEIN NJITANGO

02 JUNE 1996 MAJIRA YA JIONI PALE LUGALA HOSPITAL MALINYI ULITUACHA WANAO, MUMEO,WAJUKUU,NDUGUZO NA MARAFIKI.

SIMANZI,HUZUNI,VILIO NA SALA ZA MAOMBOLEZO KATIKA KIJIJI CHA KIPINGO ZILIAMSHWA MARA TU BAADA YA TAARIFA KUWA SAINA(AGNES) NJITANGO WA NONGWA UMEIGA DUNIA....

MENGI YALISEMWA NA MENGI YANAKUMBUKWA JUU YAKO NA YATADUMU KATIKA KUMBUKUMBU ZETU HAPA DUNIANI NA HUKO ULIKO SIKU TUTAPOONANA KATIKA ROHO, MUNGU ALIAMUA HAYO NA NI YEYE TU TUNAYEMUOMBA AKUJAALIE YOTE YA HERI.

KAMA UZAO WAKO TUNAONA FAHARI KUKUKUMBUKA MAMA YETU,MPENZI WETU NA RAFIKI WA KWELI SAINA AGNES BINT WA HUSEIN NJITANGO NA TULAHALA MBANYUKA; NYOTE MLALE KWA AMANI YA MUNGU BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU AMINA.

KESHO TUNAAZIMISHA SIKU YA KUZALIWA MJUKUU WAKO BENJAMIN NA KWA HILO MIMI NA MKE WANGU TUMEOMBA MISA YA SHUKRANI MJINI MAFINGA-IRINGA KWA HESHIMA YAKO MAMA SAINA AGNES NJITANGO, MAMA MKE WANGU BI SEVERINA KANGALAWE NA BABA WA MKE WANGU MZEE HALFAN MWINYIERIAFYA MLONGANILE...NYOTE TUNAWAOMBEA RAHA YA MILELE,PUMZIKO LA AMANI NA MWANGA WA MILELE KWENU NA SISI VIJANA WENU.

ATUBARIKI MUNGU BABA,MWANA,ROHO NA TUJAALIWE UVULI WA MAMA YETU MWENYE HERI BIKIRA WA DAIMA MARIA. AMINA.

NA FAMILIA YA BWANA NA BIBI N&V NONGWA DSM NA MAFINGA-IRINGA