‘Msitumie misikiti kuchochea chuki’


Dar es Salaam. Viongozi wa dini ya Kiislamu,  wametakiwa kuhakikisha kuwa taasisi wanazoziongoza hazitumiki kuwashawishi waumini wao kushiriki katika vitendo vya kueneza chuki, vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani.

Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary (IBIF) , wakuu wa taasisi, walimu wa madrasa na maimamu, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Khalifa Khamisi alisema hali ya utulivu imeanza kutoweka kwa sababu baadhi ya misikiti imegeuzwa kuwa viwanja vya mapambano na mahubiri yanayoeneza chuki.
Alisema kuna vikundi vichache vilivyoibuka hivi karibuni na kutumia ubabe kunyang’anya misikiti ya madhehebu mengine yanayotofautiana na yale wanayoyaamini wao.
“Kundi hili ni mfano mbaya katika makundi ya kiimani lisilokuwa na uvumilivu,” alisema.