HABARI

Na Godfrey Kahango, Mbarali. (email the author)

Posted Ijumaa,Mei24 2013 saa 21:56 PM

KWA UFUPI


  • Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wametoa mapendekezo yao juu ya mchakato wa kuugawa Mkoa wa Mbeya, ili kupata mikoa miwili kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wametoa mapendekezo yao juu ya mchakato wa kuugawa Mkoa wa Mbeya, ili kupata mikoa miwili kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Mchakato huo unakuja baada Serikali ya Mkoa wa Mbeya, kumwomba Rais Jakaya Kikwete kuugawa mkoa huo, ili kutoa unafuu kwa watendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Habari zilisema tayari Rais Kikwete ameridhia maombi hayo na kuagiza kufanyika kwa mchakato huo.

Kw upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka madiwani wa hamashauri zote kuketi na kuanza mchakato wa mapendekezo kuhusu namna ya kuugawa mkoa huo.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali walitoa mapendekezo yao juzi katika kikao chao.

Akisoma taarifa ya mapendekezo hayo katibu wa baraza hilo, Brown Mwakibete, alisema timu

ya wataalamu iliketi na kutafakari kwa kina namna ya kuugawa mkoa huo kwa kuzingatia maagizo ya mkuu wa mkoa.

Diwani Mwakibete, alisema madiwani wa halmashauri hyo wamependekeza jina la mkoa mpya liwe Rungwe ukiwa na Wilaya za Kyela, Rungwe,

Ileje na Mbozi na makao makuu ya yawe Tukuyu.

Alisema pia wametaka jina la mkoa wa zamani libaki kuwa Mbeya ukiwa na Wilaya za Momba, Chunya, Mbeya na Mbarali na Makao makuu yakiwa Mbeya.

Alisema kamati hiyo haikuona haja yaa kuanzisha wilaya mpya kutokana na sababu za kijiografia.