Tanzia :Jaji Mwaipopo afariki dunia kwa ajali ya gariAnazikwa leo kijijini kwao Igowole -Mufindi Iringa


Mrehemu Jaji Mstaafu Ernest Mwaipopo enzi za uhai wake           Morogoro
JAJI Mfawidhi wa Divisheni ya Mahakama ya Kazi ya Mahakama Kuu, Msaafu Ernest Mwaipopo amefariki katika ajali iliyotokea Mkoani Morogoro leo alipokuwa akirejea Dar es Salaam kutokea Mkoani Iringa. 
Hayo yameelewa na mtoto mdogo wa marehemu LukeloMkami  Mwaipopo  alipozungumza na mtandao wa www.francisgodwin. blogspot.com ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo wakati  akitokea  mkoani Iringa.
Lukelo amesema  kuwa katika gari  hiyo  walikuwepo  watu  watano pamoja na dereva na  kuwa chanzo  ajali hiyo kinatajwa  kuwa ni kupasuka kwa taili la mbele.
Hata  hivyo alisema  kuwa  taratibu  za mazishi zitafahamika baada ya mwili  huo kupelekwa  jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya taratibu  za mazishi yatakayofanyika katika wilaya ya Mufindi.
Jaji Mwaipopo alistaafu rasmi Oktobar 08 mwaka 2010 na kuagwa rasmi, Jaji Mwaipopo alikuwa kati ya majaji mahili na waliofanya kazi kwa uadilifu mkubwa nchini.