KARIBU ULANGA MAGHARIB KANALI KINANA...TUNAOMBA WILAYA MPYA YA MALINYI

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI COL. ABDULAHMAN KINANA.

JUMATATU YA TAREHE 15 KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI ATAKUWA TAYARI MKOANI MOROGORO KWENYE WILAYA TARAJIWA YA MALINYI,;

NINI KILIO CHENU WANA ULANGA MAGHARIBI/MALINYI?

DARAJA MTO KILOMBERO-UJENZI UHARAKISHWE
BARABARA YA SONGEA-MPANGO ENDELEVU UWEPO SASA
WILAYA MPYA YA MALINYI-ITANGAZWE NA MH.KIKWETE KABLA HAJAAGA IKULU LAKINI CCM YENYEWE WATUMIE FURSA HII KUITANGAZA WILAYA YA KICHAMA YA MALINYI...
UMEME-MRADI UMEDUMAA ...SIASA ZIWEKWE PEMBENI TUPATE UMEME
Huduma za jamii na mambo mengine yatakuja automatically....jamii tuitumie fursa ya kisiasa kuishinikiza CCM kuzikubali hoja zetu na siyo hoja za viongozi wachache ambao usiku huu wa tarehe 13/04/2013 wako tarafani Mtimbira wakiratibu ujio wa Katibu Mkuu wa CCM jimboni Ulanga Magharibi...ilihali makao makuu ya jimbo yako Malinyi!!! Huu ni uhuni.

Mkutano huu kufanyika Mtimbira ni agenda mahsusi ya Mh. Mponda kuiandaa Mtimbira kuwa HQ ya wilaya  tarajiwa hilo kiuchumi, kisayansi,kimazingira na hata kihistoria ni wazo potofu sana... na ni kosa kubwa kisiasa ambalo litaigharimu CCM kwa miongo mingi sana ijayo, mfano ni kama tuwaonavyo wa Lutheri Ulanga Kilombero walivyopoteza dira. Historia ni mwalimu na mwalimu bora ni historia...Malinyi ni historia isipuuzwe

Jamii ya Ulanga Magharibi watambue kuyaweka makao makuu Malinyi ni kuihakikishia wilaya tarajiwa yote fursa sawa kwa mujibu wa Policy ya nchi yetu....kila huduma za muhimu ni lazima zifike makao makuu ya Wilaya.

Tunawaomba CCM waliangalie jambo hili kwa umakini na uzito wake, lakini ni lazima watambue mchango wa kihistoria ambao Malinyi umetoa tangu harakati za uhuru , TANU na CCM na zama hizi za mageuzi.
 Malinyi ni mama na mwalimu wa historia asipuuzwe.

Karibu Malinyi Mheshimiwa Kanali Mstaafu Abdulahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM