EDUARD MORINGE SOKINE SHUJAA ASIYECHUJA ....WAZIRI MKUU DAIMA MIOYONI MWA WATANZANIA

Naikumbuka April  12, 1984 nikiwa kijijini Kiswago nikiwa na umri wa miaka 11 na mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kiswago...nikiwa naaishi kwenye nyumba za walimu ilikuwa wazi 277 haikukosekana licha ya kuwa mazoea na Radio ni ya tangu utotoni nikiwa na baba mzazi wangu Balozi wa nyumba kumi na mpambe muhimu wa M/kiti wa CCM zama hizo pale kijijini Kipingo mjini Malinyi-Ulanga, iliendana na mapumziko ya nusu muhura na pasaka majira ya saba kwenda saa nane mchana nasikia wimbo wa Taifa ambao kwa mazoea ni saa kumi na mbili asubuhi na saa sita za usiku nikiweza wakati RTD inafungwa ndio lazima usikike...wakubwa pale kwenye kota za waalimu wakasema wekeni Radio vizuri kuna jambo hapo!!! Ni kweli alikuwa ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa Ikulu anautangazia Umma wa Tanzania kifo cha Waziri Mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine....nakumbuka neno " Kijana wetu" lilivyotamkwa na Mwalimu Nyerere kuonyesha uzito wa maumivu na pigo alilopata yeye na nchi....sintaisahau siku ile maana pale Kiswago iliendelea na mvua mpaka siku anazikwa Marehemu Sokoine...kama Kiswago,Malinyi,Mtimbira ilizizima vile kwa kifo cha kiongozi ambaye hawakuwahi kumuona Ulanga yote zaidi ya kumsikia akirindima redioni na magazetini .....Marehemu Edward Sokoine ni Waziri mkuu pekee katka watatu wa mwanzo wa nchi hii ambaye hajawahi vuka mto kilombero....na kuvuka kimwili kwenda Ulanga lakini alivuka mto huo mioyoni kwa matendo yake....Mungu ampe pumziko la amani
Malinyileo.


KUTOKA JAMIIFORUMS.....

Default Namkumbuka Edward Moringe Sokoine!

Edward Moringe Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini akishika wadhifa huo mara mbili ktk vpnd tofauti.Uongozi wake ulikuwa mfano kutokana na uadilifu wake,ufuatiliaji wake kwa viongoz huku akikemea rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.Namkumbuka kwa mambo mawili makubwa kwangu mim.1.Alipokuwa kwenye ziara zake za kikazi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani alipita shule moja ya msing alikuta wanafunzi wamemsubir tang asbh na muda huo ilikuwa saa tisa,akiwa na msafara wake akauliza "Hivi watoto hawa wamenisubiri tang saa ngap?akajibiwa tang asbh.Akuliza "Wameshakula?" hakupata jibu.Akasema mimi narejea dar na hvyo kila m2 akale kwake,hiki chakula wapeni watoto wale.2.Alikataa kuitwa mheshimiwa yeye na Mwalimu na walipenda kuitwa ndugu.Wakiamini kama kuna mh. pia kutakuwa na mdharauliwa.Nani anaweza kuwajal wanafunz kama alivyofanya yeye?Siku waheshimiwa ni weng madiwan,mwenyekiti mpaka ma baamedi.Sokoine alipinga kutukuzwa.Huyu ndio Edward Moringe Sokoine ninaemkumbuka.Hakika hakuna kama yeye kizazi hiki.

IBADA YAKE WAMI DAKAWA LEO

PICHA ZA IBADA YA KUMUOMBEA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINEKWA HISANI http://ladyjaydee.blogspot.com/2012/04/picha-za-ibada-ya-kumuombea-hayati.html

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( kulia) akisalimiana na Askofu Telesphor Mkude , ( kushoto) baada ya kumaliza kusoma ibada ya misa ya  kumkumbuka  ya kumwombea Marehemu , Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine , aliyetimiza miaka 28 tangu kifo chake kilichotokea Aprili 12, 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Pinda alikuwa ni mgeni rasmi katika tukio hilo.
Waziri Mkuu wa zamani aliyejihudhuru Edward  Lowassa ( kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe , baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kanisa la Kigango cha Wami Sokoine , kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 28 ya Kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine , kilichotokea Aprili 12, 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya watoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine , aliyekuwa Waziri Mkuu,ambaye alifariki dunia Aprili 12, mwaka 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, miongoni mwa watoto hao ( wakwanza kulia ) ni Mbunge wa Viti Maaalumu, Namelok Sokoine.

Pichani chini ni
Mbunge wa jimbo la Mvomero Bw. Amos Makalla akisalimiana na Askofu mara baada ya misa hiyo kumalizika
Somebody Not Hater: said...
Jaman mbona hii ibada hata haijavuma?!!!watu Kanumba Kanumba kwel Kanumba nuksi.
Anonymous said...
HII NI IBADA ZA MIZIMU HAKUNA KWENYE MAANDIKO POPOTE INASEMA TUWAOMBEE MAREHEMU.MAANDIKO YANASEMA UNAPOKUWA HAI TENDA MAMBO YAKO YOTE NA KUTENDA MEMA HATA UKIFA UWE NA TUMAINI LA UFUFUO WA KWANZA. KAMA HAKUTENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU WAKATI YUKO HAI HAITASAIDIA KITU WAKATI AMEKUFA NA KUOMBEWA ETI MUNGU AMUWEKE PEMA PEPONI...HATA AKIOMBEWA KUMBUKUMBU ZAKE ZOTE ZIMEFUNGWA.NA HAWASIKII WALA HAWAELEWI HIVYO SOMENI MAANDIKO MPATE MAARIFA YA KUJUA MUNGU ANAHITAJI TUFANYE NINI.WATAANZA HADI KUMSUJUDIA SASA HUKO TUNAKOKWENDA MAANA WANASEMA ETI NI MTAKATIFU JE ULIJUA MAHUSIANO YAKE NA MUNGU YAKOJE HADI AITWE MWENYEHERI?????SOMENI MAANDIKO YATAWAWEKA HURU KWELI KWELI.
Anonymous said...
HII NI IBADA ZA MIZIMU HAKUNA KWENYE MAANDIKO POPOTE INASEMA TUWAOMBEE MAREHEMU.MAANDIKO YANASEMA UNAPOKUWA HAI TENDA MAMBO YAKO YOTE NA KUTENDA MEMA HATA UKIFA UWE NA TUMAINI LA UFUFUO WA KWANZA. KAMA HAKUTENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU WAKATI YUKO HAI HAITASAIDIA KITU WAKATI AMEKUFA NA KUOMBEWA ETI MUNGU AMUWEKE PEMA PEPONI...HATA AKIOMBEWA KUMBUKUMBU ZAKE ZOTE ZIMEFUNGWA.NA HAWASIKII WALA HAWAELEWI HIVYO SOMENI MAANDIKO MPATE MAARIFA YA KUJUA MUNGU ANAHITAJI TUFANYE NINI.WATAANZA HADI KUMSUJUDIA SASA HUKO TUNAKOKWENDA MAANA WANASEMA ETI NI MTAKATIFU JE ULIJUA MAHUSIANO YAKE NA MUNGU YAKOJE HADI AITWE MWENYEHERI?????SOMENI MAANDIKO YATAWAWEKA HURU KWELI KWELI.