Mholanzi aliyekuwa na chuki dhidi ya Uislamu asilimu

http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/30147-mholanzi-aliyekuwa-na-chuki-dhidi-ya-uislamu-asilimu

Mholanzi aliyekuwa na chuki dhidi ya Uislamu asilimu


Ukurusa wa tiwtter wa Mholanzi aliyesilimu  Arnoud van Doorn Ukurusa wa tiwtter wa Mholanzi aliyesilimu Arnoud van Doorn
Mwanasiasa maarufu wa Uholanzi ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa chuki dhidi ya Uislamu sasa amesilimu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IQNA, Arnoud van Doorn ambaye alikuwa katika chama kimoja na  Geert Wilders Mholanzi mwenye chuki dhidi ya Uislamu sasa amesilimu baada ya kuutambua Uislamu kama njia ya haki maishani.
Tovuti ya islamic-events.be imechapisha taswira ya akaunti ya ukurusa wa kijamii wa twitter wa  van Door chini ya anuani ya 'mwanzo mpya' ambapo pia shahada mbili zimeandikwa akwa lugha ya Kiarabu.
Awali ilikuwa vigumu kwa Waislamu wengi Ulaya kukubali kuwa mwanasiasa huyo aliyekuwa na chuki dhidi ya Uislamu amesilimu lakini von Doorn mwenyewe  amethibitisha ukweli wa habari za kusilimu kwake. Amesema kukubali kwake Uislamu ni suala binafsi na hivyo kwa sasa hataki kulijadili zaidi.