Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Tunampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea yeye na timu yake.