Awali ya yote namshukuru mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa fursa ya kupata elimu ambayo bila shaka ninalo deni kwa wananchi wa Mufindi,mimi nimezaliwa kijiji cha kihanga,wilaya mufindi,mkoa wa Iringa leo nitagusia kwa ufupi mambo matatu ambayo yapo mufindi lakini bado watu wake ni maskini
(1)SHAMBA LA MSITU WA SAOHILL
(2)SHAMBA LA CHAI UNILIVER
(3)KIWANDA CHA KARATASI MGOLOLO(MPM)
Bila woga nataja hadharani kuwa ufisadi uliokidhiri ktk shughuli hizo muhimu hazijaweza kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika kutokana na vingozi wakubwa na wilaya kuingia mikataba ya kifisadi na kujimilikisha rasilimali kwa njia isiyo halali mfano WAZIRI LUKUVI MB(ISIMANI) anamiliki kitalu cha miti kupitia kiwanda cha ustas karibu na kiwanda cha nguzo za umeme ambacho kinamilikiwa na MERAB KIIJIJI CHA KIHANGA.
Mkuu wa wilaya EVARISTI KALALU ana kibali kupasua mbao isivyo halali,pia amejimilikisha ardhi kimabavu ktk kijiji cha Mapanda.
Kiwanda cha Mgololo limekuwa shamba la bibi na amemiliki MNORWAY miaka(90),wafanyakazi hawajalipwa stahiki zoa tangu kubinafsishwa kiwanda miaka zaidi ya kumi na mbili sasa.

Mashamba ya chai balaa tupu mshaharaTsh 3000@siku mabadiliko ni sasa