CHINA YA RAIS Xi JINPING ILIPOREJA UPYA TANZANIA 2013 BAADA RAIS Hu

http://issamichuzi.blogspot.com/2013/03/rais-kikwete-na-rais-xi-jinping-waweka.html

Rais Xi Jinping wa China awasili Tanzania


Rais Xi Jinping wa China leo amewasili nchini Tanzania kuanza safari yake ya kuzitembelea nchi tatu za Afrika.
Akiwa nchini Tanzania, anatarajiwa kusaini mikataba 17 na serikali ya nchi hiyo, kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Tanzania.
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa, Rais Jinping ambaye alichukua hatamu za uongozi Machi 14 nchini China ataonana pia na viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo.
Mbali na Tanzania, Xi Jinping atazitembelea pia nchi Afrika Kusini na Congo Brazzaville.
Akiwa Afrika Kusini, Jinping atahudhuria mkutano wa kundi la BRIC linalojumuisha nchi 5 zinazokuwa haraka kiuchumi. Nchi hizo ni pamoja na Brazil, India, Afrika Kusini, China na Russia.
Rais mpya wa China alikuwa nchini Russia kuanzia mwishoni mwa wiki ambako alisaini mikataba kadhaa ya ushirikiano na serikali ya Moscow. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, umuhimu wa bara la Afrika kwa China ni sababu iliyopelekea kiongozi huyo kuchagua bara hilo kama kituo chake cha pili kukitembelea katika safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipochukua hatamu za uongozi.
http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/30713-kuhusu-safari-ya-rais-wa-china-nchini-tanzania
  • Kuhusu safari ya Rais wa China nchini Tanzania
  • China kuimarisha mashirikiano na nchi za Kiafrika

    China kuimarisha mashirikiano na nchi za Kiafrika

    Zhai Jun Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa China Zhai Jun Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa China
    Zhai Jun Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa China amesema kuwa, China ina azma kubwa ya kuimarisha zaidi mashirikiano yake na nchi za Kiafrika.  Zhai Jun ameyasema hayo wakati wa kukaribia safari ya Rais Xi Jinping wa China ambaye atazitembelea nchi za Tanzania, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hali kadhalika Rais mpya wa China anatazamiwa kushiriki kwenye kikao cha wakuu wa kundi la BRICS nchini Afrika Kusini, kundi ambalo linazishirikisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Hivi karibuni Makamu wa Rais wa China alisema kuwa, kuna Wachina milioni moja na nusu pamoja na maelfu ya mashirika ya Kichina yanayofanya shughuli za kibiashara barani humo. Imepangwa kuwa Rais Jinping wa China atafanya safari katika nchi hizo tatu za Kiafrika kuanzia tarehe 22 hadi 31 za mwezi huu. Hii ni safari yake ya kwanza kulitembelea bara la Afrika tokea achukue wadhifa wa kuliongoza taifa hilo hivi karibuni.