Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi - STAR TV leo asubuhi, Prof Lipumba amedai kuwa sera mbovu za Mwl Nyerere ndizo zilizodidimiza uchumi wa Tanzania.
Chanzo: sangu mnene:http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/384623-prof-lipumba-matatizo-ya-tanzania-yamechangiwa-na-sera-mbovu-za-mwl-nyerere.html
sangu mnene
Naomba msaada wenu wana Jf, hivi sera mbovu ni zipi? Mwl Nyerere alijenga viwanda, Waliokuja wakabinafsisha.

Mwl aliimarisha TANESCO kwa kujenga mabwawa, waliokuja wakaacha kujenga mabwawa wakaanzisha umeme wa mafuta.

Mwl aliupinga ufisadi, waliofuata wakaanzisha Takrima.

Mwl alijenga nyumba za wafanyakazi, waliofuata wakaziuza.

Mwl aliwajali wakulima kwa kuwapatia soko la uhakika la mazao yao na kuwapatia elimu ya kilimo na pembejeo kwa bei ndogo, waliofuata wamewaacha wakulima wakisota na kila wakipata soko la nje wanazuiwa.

Mwl alijitahidi kutoa huduma bora za jamii bure, waliofuata wanazigawa kwa matajiri tu.

Mwl aliimalisha shirika la Reli na kujenga TAZARA, waliofuata wakauza kwa wahindi.

Mwl alizuia migodi kuchimbwa kiholela na wageni,waliofuata wakaigawa kwa wageni.

Mwl aliweka miiko ya uongozi, waliofuata wakaiondoa.

Mwl alijenga umoja wa kitaifa kwa kupinga ukabila na udini, waliofuata wameanza kuiondoana huenda kwenye katiba mpya serikali ikawa na dini, na mengineyo mengi.

Hivi Prof anazeeka vibaya au ana chuki binafsi na BABA WA TAIFA? Naomba ufafanuzi toka kwenu, yapi mabaya aliyoyafanya Mwl Nyerere ambayo viongozi waliomfuatia waliyatekeleza vema?

Malinyileo imelazimika kuiweka habari hewani ili tupate japo maoni ya wadau na wapenda maendeleo. Kwa kuanzia nawaweka wachangajiaji wa mwanzo wa JF na maoni yao pengine watupe mwanga juu ya madai haya ya Associate Professor Ibrahim Haruna Lipumba-M/kiti wa CUF

Maoni ya wana Jamiiforums.com
 
Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

Ujamaa ilikuwa SERA mbovu na ndio chanzo cha umasikini wa nchi. Hata CHINA wameanza kujikomboa baada ya kuupa kisogo ujamaa! However, unaruhusiwa kumpenda NYERERE

 mv butiama

Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

Lipumba ana chuki binafsi na Mwalimu Nyerere ambae hivi karibuni anategmewa kuwa mwenye heri baada ya kufanya kazi kubwa ya kutengeneza mfumo ambao hivi sasa taifa unaitafuna
 MKANKULE

Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

ujamaa ni sera na mfumo ambao kuendelea kwake ni kazi sana.nchi zote zilizoendelea zilifuata mfumo wa kibeberu hata kenya ndugu zetu wanatupita kwakuwa wamefuata ubepari
 
sifongo's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 5th June 2011

Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

tenda wema uchape lapa usitegemee waswahili waje wakupe asante au kukusifu.
 1. #6
  paul vicent's Avatar
  1

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Anazeeka vibaya
 2. #7

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Ujamaa ndo mfumo mbovu iliyowahi kutokea dunia.Kwa hili nyerere hana cha kukwepa.Ila kwa mambo mengine anastahili sifa hasa kwa upande wa maadili kwa viongozi
 3. #8

  Default Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Hivi kumbe kuna TV Tanzania !?
  JK Ni Rais wa watu mil.5 kwenye nchi ya watu mil.50 (By vote)

 4. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Quote By Utamaduni View Post
  Hivi kumbe kuna TV Tanzania !?
  Anawazimu huyu!!!Yeye mwenyewe alisomeshwa na nyere baada ya kutaifisha shule za wakristo na ametibiwa na mahosipitali ya kikristo mpaka leo kwa amri ya serikali ya nyerere isiyo na ubaguzi wa dini wala kabila...Ndo maana mkapa alisema huyu ni profesa njaa aka kanjanja
  August, Mupirocin and Jacobus like this.

 5. 25

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  dah we lipumba wewe! nyerere kwetu ni kama malaika huwa hakosei.We unamlaumu mtu ambaye ni mwenye heri tunataka kumfanya awe mtakatifu.Ngoja waje wenyewe watakavyokushukia kwa jazba
  mwanaharakati5 likes this.
 6. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Haya ndo yalisemwa na mkapa ni kweli walifanya makosa hata nyerere alikosea lakini kimefanyika nini kurekebisha zaidi ya kulaumu kizazi cha digital ndo kinaharibu zaidi, turekebshe tuache kulialia tuu!
  August likes this.
  TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

 7. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Mtazamo hapa ni sera na Ujamaa ndizo zilikuwa bapa sana mkuu!
 8. kpm is offline
  kpm

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Kumlaumu Nyerere wakati huu ambapo tangu atoke madarakani mwka 1985 si sahihi, tungekua tunasema ni nini kizuri kimefanyika miaka hii yote ambayo Rais hakuwa Nyerere! Kulaumu historia hakusaidii lolote!
  August and Jacobus like this.
 9. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Lipumba nina wasiswasi na uprofesa wake, kama alidhani ubepari ndio mzuri, akawauliza former Zaire, sasa DRC, walianza ubepari baada ya uhuru, lakini maendeleo yako Kinshasha tu, sasa Lipumba anaponda sera za Nyerere leo?

  Lazima kuna la ziada ambalo Lipumba atakuwa nalo juu ya hayati Mwl.JK
  August likes this.
 10. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Ni upumbavi kabisa kusema matatizo yete yanatokana na Nyerere! jamani alikuwa kiongozi wa nchi kwa miaka 23, ....tangu atoke madarakani ni zaidi ya miaka 25.... sasa sisi ndio wajinga au nani?...akina Lipumba ni wavivu wa kufikiria tu,

  Quote By kpm View Post
  Kumlaumu Nyerere wakati huu ambapo tangu atoke madarakani mwka 1985 si sahihi, tungekua tunasema ni nini kizuri kimefanyika miaka hii yote ambayo Rais hakuwa Nyerere! Kulaumu historia hakusaidii lolote!
  August and CHIGANGA like this.
 11. #16

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Sera za Nyerere kwenye uchumi zilishindwa vibaya.
  Ndallo and mwanaharakati5 like this.
 12. #17

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Quote By Gwakisa Mwandule View Post
  Anawazimu huyu!!!Yeye mwenyewe alisomeshwa na nyere baada ya kutaifisha shule za wakristo na ametibiwa na mahosipitali ya kikristo mpaka leo kwa amri ya serikali ya nyerere isiyo na ubaguzi wa dini wala kabila...Ndo maana mkapa alisema huyu ni profesa njaa aka kanjanja
  Mwenda wazimu si kidogo. Kijijini kwao Ilulangulu ni mfano wa huyu jamaa. Kikwete anapafahamu.
  Tafakari kwanza kabla....................
 13. #18

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  mi nafikiri ungekuwa unajibu hoja alizozitoa kwa kuonyesha ubovu huo wa sera na mfumo, mi pia nakubaliana na lipumba tupo hapa kwa sababu ya nyerere
 14. #19

  Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Quote By andrewk View Post
  Ni upumbavi kabisa kusema matatizo yete yanatokana na Nyerere! jamani alikuwa kiongozi wa nchi kwa miaka 23, ....tangu atoke madarakani ni zaidi ya miaka 25.... sasa sisi ndio wajinga au nani?...akina Lipumba ni wavivu wa kufikiria tu,
  Hizi mnasahau kuwa sasa hivi nchi hii chama tawala ni CCM/CUF? (serikali ya umoja ya kitaifa).
  Tafakari kwanza kabla....................
 15. Default Re: Prof Lipumba: Matatizo ya Tanzania yamechangiwa na sera mbovu za Mwl Nyerere

  Quote By Manyi View Post
  Mtazamo hapa ni sera na Ujamaa ndizo zilikuwa bapa sana mkuu!
  Wewe hebu fikiri kidogo tu. Huoni kuwa sera hizo zimedumisha walau utu wa mtanzania hadi majuzi? Ni nchi gani ya kiafrika iliyofuata mfumo wa kibepari mara baada ya ukoloni ambapo mwananchi wa kawaida anamiliki ardhi yenye rutuba? Sera hizo zilikuwa muafaka kwa kuanzia mara baada ya uhuru, vinginevyo baadhi yetu neno shule (elimu) lingekuwa msamiati kwetu. Tchao.
  August and CHIGANGA like this.
  Malinyileo tunapingana kwa asilimia 100% na madai ya mwanazuoni huyu na sasa mwanasiasa. Kwanza nawaomba tukubaliane kuwa  hakujawahi kuwapo na sera za Mwalimu Nyerere bali sera ya Tanganyika -Tanzania huru chini ya uongozi wa  Mwal.Nyerere, hapa tunamaanisha kuwa maamuzi yote yalikuwa ya Watanzania na si ya mtu mmoja. Kufauru kwetu na kushindwa kwetu ni matokeo sawa kwetu sote akiwemo Lipumba. Ni jukumu la wasomi kuisaidia nchi kimaono, kujitoa muhanga ili kuleta maendeleo ya kweli, na kushiriki kwa  dhati katika kila tunalokubaliana kama nchi na siyo vinginevyo. Tujiulize kama Lipumba na wale wanaomlaumu Nyerere walithubutu kujenga hoja makini na kushawishi serikali na wananchi ktk maono yao? Kinyume cha hapo ni unafiki ila tutambue kila mwananchi ana agenda kuu ktk kuleta maendeleo ya kweli. La muhimu na ni lazima kwetu kama Wana wa Tanzania ni kutambua wajibu wetu wa msingi ni kuamini  " Tanzania kwanza"