‘Lulu’ ruksa kuingia uraiani leo au kesho pindi atakapotimiza masharti matano ya mahakama

 

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja anatakiwa kudhamini kiasi cha shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo, hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia January 29, 2013 ambayo ni kesho, kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.