JE MOROGORO HAIPASWI KUGAWANYWA?

Nangojea kwa hamu siku Rais atakapotangaza kuwa Morogoro imegawanyika katika mikoa miwili, wa morogoro na Kilombero huku kwa upande wa Mkoa mpya wa Kilombero Utakuwa na wilaya za Kilombero, Ulanga, Ulanga Magharibi na Mlimba, maana kwa sensa ya 2002, mkoa wa morogoro ulikuwa na watu wengi kuliko mkoa wa Iringa
Malinyi leo inawataka wadau mbalimbali kuzingatia taarifa mbalimbali ktk kukubaliana au kupingana na ndg.Mahundo katika hoja yake juu ya ndoto ya Kilombero/Ulanga region na Morogoro region........

Wilaya ya Ulanga peke yake ni kubwa zaidi ya Mkoa wa Kilimanjaro !!! Wana Kilimanjaro wengi wako nje ya mkoa wao kuliko wakazi wa mikoa mingine!!! kamahoja ni ukubwa wa eneo ama idadi ya watu kwanini Malinyi isiwe wilaya ama Ulanga usiwe mkoa mpya?

Tujipange kwa hoja, siasa na uzalendo wa kujiletea maendeleo.....kumbukeni Mwalimu Nyerere na falsafa ya Madaraka Mikoani ......Alimaanisha na ndio maana Mh.Rais wa awamu ya nne anatenda kwa uangalifu mambo haya.....

Tuungane na tuwaunge mkono viongozi wetu kwa hoja na maono jengefu.....