Diwani wa ccm adaiwa kufumaniwa – ang’olewa meno, akatwa sikio

Default Diwani wa ccm adaiwa kufumaniwa – ang’olewa meno, akatwa sikio

Diwani wa CCM wa Kata ya Ifunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijjini, katika Jimbo la Kalenga, Eliya Mngwila, anadaiwa kufumaniwa na mke wa jirani yake juzi usiku kasha kukatwa sikio la kulia na kung’olewa meno matatu kwa kipigo.
Dawina huyo anadaiwa kufumaniwa na mke Daima Msigala, mkazi wa Kijiji cha Ifunda. Inadaiwa kuwa wakati wa fumanizi hilo diwani huyo alishambuliwa kwa marungu, hatua iliyosababisha meno yake matatu kung’oka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Micheal Kamuhanda, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Ni kweli diwani, Eliya Mngwila (48), alifumaniwa kwenye nyumba ya Daima Msingala majira ya saa 7.00 usiku, ambapo na jina la mwanamke aliyefumaniwa naye, limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama”, alisema Kamanda Kamuhanda.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 16, mwaka huu, katika Kijiji cha Ifunda, tarafa ya Kiponzero. Diwani alipigwa kwa marungu na kujeuriwa, baada ya kumfumania na mke wake (Msigala) – anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la Majira’ Alhamisi, Januari 17 ,2013


Naomba nikiri kuwa nina sababu kuu mbili za kuiweka hii habari hapa; Mosi  nimeiweka ili jamii ione namna ya wenye madaraka,mamlaka na fursa za kujuana na watawala,fedha na hata wasaidizi tu wa wenye mamlaka wanavyoenda mbali ktk kuonea wananchi wanyonge mpaka kuwapora hata ndoa zao,wake zao, mali zao na utu wao. Pili nalazimika kuiweka habari kwa kurejea historia 1988 pale mmoja wa wapishi wetu wa Ifunda technical Sec School alipouawa ktk mashamba ya mahindi kuelekea kwa mzee Mwaitebela akiwa anafanya ngono na mke wa mtu. Mwenye mke alipotonywa aliwafuatilia nyuma na kumuua mgoni wake. Tunalo la kujifunza hapo wananchi. Kwanini Ifunda? Kwanini wenye fursa za kisiasa,dola na mamlaka? Tubadilike hii ni laana.
By:Malinyileo.