CCM NA WAPINZANI WAKIWA KAZINI...SI MCHEZO...WANA JAMII NAO WAKO KTK HARAKATI...HII NDIO TANZANIA TUNAYOITAKA.....

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana akihutubia ngaruka
 Dk Asha-Rose akihutubia Nguruka
Nape Nnauye akihutubia Ngaruka
Kinamama katika mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wakipokea kwa shangwe msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
 Juma Kilabuka na Hasani Kankwi wa mjini mdogo wa Nguruka wakifurahia msafara wa Kinana ulipofika katika mji huo
Kinana akisalimia wananchi katika mji mdogo wa Nguruka , Uvinza mkoani Kigoma baada ya msafara wake kuwasili  katika mji huo kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka,  Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili Nguruka mkoani Kigoma, Januari 28, 2013.
Kinana akiaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka, wilayni Uvinza mkoani Kigoma. Kushoto kwake ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
Dk. Asha Migiro akiwa katika matembezi kuingia mjini mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM. Kushoto ni Asha Baraka.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kwenda kwenye mkuytano wa hadhara wa CCM, Nguruka, Januari 28, 2013. Pembeni yake ni Asha Baraka
Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akimtembeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na ujumbe wake kushuhudia hali ya ujenzi wa daraja hilo ilivyo, Januari 28, 2013, wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa You mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika  Aprili mwaka huu. Wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kushoto) . Kinana na ujumbe wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Januari 3, 2013.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Khalidi wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kushoto ni  Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Yong.Picha Zote na Bashir Nkromo-Idara ya itikadi na Uenezi-CCM
----
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema kuwa wananchi wa Mtwara wanayo hoja hivyo Serikali inatakiwa kuwasikiliza na kutoa majibu sahihi.

Pamoja na hayo chama hicho kimesema kuwa kinachoonekana hivi sasa nyuma ya sakata hilo kuna watu wanafanya uhaini, uhalifu na kila aina ya hujumu jambo ambalo wanaitaka Serikali kuchukua hatua kali za kuhakikisha wote wanojihusisha na uhalifu huo wanachukuliwa hatua.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ikiwa ni msimamo wa chama chao katika sakata hilo.

Mjadala wa gesi ya Mtwara kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam umekuwa gumzo kubwa huku wananchi wakiitaka Serikali kuwaeleza watanufaika vipi na gesi hiyo kabla ya kunufaisha maeneo mengine.

Kinana alisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuhakikisha inatumia nafasi yake kuzungumza na wananchi wa Mtwara katika kupata suluhu ya suala hilo kwani wana hoja za msingi ambazo zinataka majibu.

“Msimamo wetu kama chama, tunataka Serikali kukaa na wananchi hao na kuwasikiliza.Tunahitaji kuona Serikali inatoa majibu ambayo yatakuwa sahihi na kumaliza tofauti iliyopo sasa,”alisema Kinana.

Pamoja na hayo alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona hali ya uvunjifu wa amani inayofanywa na baadhi ya watu ambao wameamua kuingia mtaani na kuiba, kupora mali na kuharibu nyumba za watu kwa kuzichoma moto.

Alisema kuwa CCM inaona ni wakati mzuri kwa Serikali kuwadhibiti wote ambao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu huo ambao haukubaliki huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kusikilizwa.

Alisema mtazamo wa chama chao ni kwamba kuna jambo ndani ya suala hilo maana gesi inatakiwa kujadiliwa kwa njia ya amani kupata suluhu kuliko mali za watu kuharibiwa na kufanywa kwa uhalifu ambao hauvumiliki.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat-ulamaa) Shk. Suleiman Amran Kilemile Akitoa Nasaha Juu ya Umuhimu wa Waislam Kiimarisha utekelezaji wa Ibada ya Kutoa Zakat kwa Makundi yaliyotaja Katika Qur’an kwani ndio Njia rahisi ya Kuimarisha Uchumi wa Jamii na Nchi kwa Ujumla.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Baytul -ulmaal (Charity Fund) Tanzania akisisitiza Umuhimu wa Matajiri na Wasomi wa Kiislam Kushiriki Kikamilifu kuimarisha Mfuko huo kwa Maslahi ya Ustawa wa Jamii hasa Masikini na wenye mahitaji maalum ili kuleta uiano wa kimaendeleo.
 Kijana Mfanyabiashara Ndogo Ndogo ambae amekuwa akitoa Zakat mara kwa Mara akitoa ushuhuda jinsi gani utoaji wa Zakat Umemsaidia kulinda na Kukuza Biashara yake katika Mkutano wa Ugawaji Zakat.
Kijana Mwanafunzi Yatima anayejiunga na Shule ya Serikali akipokea Tshs 100,000 Kutoka kwa Sheikh Suleiman Kilemile kama Fungu la Zakat lililotolewa Katika Ukumbi wa Lamada Ilala. Mfuko wa Baytul –ul maal Unaendeshwa pamoja kati ya Wanataalum wa fani mbali mbali za kimazingira pamoja na Wanazuoni wa Kiislam kukuzanya Zakat pamoja na Waqfu kwa manufaa ya Jamii ya Kiislam.
 Baadhi akina Mama wakifuatilia kwa Makini Mada Juu ya Utekelezaji wa Ibada ya Zakat ambayo ni Nguzo Muhimu katika dini ya Kiislam yenye lengo la kupambana na Umasikini ndani ya Jamii ya eneo husika.
Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Shk Twaha Bane wakati akieleza Umuhimu wa Waislam kuitekeleza Nguzo ya Zakat kwani inaleta Upendo, Amani na Uimara wa Biashara kwa Mtoaji na anayepokea.

  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanchama wa chama hicho aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Clemence Tara baada ya kujiunga na chama hicho.
 Katibu Mkuu Dk. Willbroad Slaa akizungumza katika mkutano huo.
 bungo John Mnyika akitete jambo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa (kulia) wakati wa Kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
  Katibu Mkuu Dk. Willbroad Slaa akisalimiana na baadhi ya wajumbe katika mkutano huo.
 Mbunge Kigoma, Zitto Kabwe akiwasikiliza kwa makini wajumbe wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kutoka mkoa wa Mtwara.
 Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei akiingia katika ukumbi wa mkutano huku akifuatana na Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe.
 Picha juu na Chini sehemu ya wajumbe wakiitikia  Peoples Power
Sehemu ya Wabunge wa Chadema
  Wajumbe wa mkutano.
 Baadahi ya wabunge wa Chadema wakiwa katika kikao hicho.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika(katikati) akiwa amepozi na baadhi ya wajumbe.Picha zote na Mdau Dande Francis

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Benno Ndulu( kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia).mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika leo jumatatu januari 28, 2013. Ujumbe huo wa BOT ulikutana na Tume na kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu (kulia)) akibadilishana mawazo na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kutoka kulia Joseph Butiku, Prof. Mwesiga Baregu (katikati), na Dkt. Sengondo Mvungi mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika leo jumatatu januari 28, 2013. Ujumbe wa BOT ulikutana na Tume na kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Benno Ndulu (kulia)akibadilshana mawazo na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kutoka kulia Joseph Butiku (kushoto)na Profesa Mwesiga Baregu (katikati) mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika leo jumatatu januari 28, 2013. Ujumbe huo wa BOT ulikutana na Tume na kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya.Picha na Tume ya Mabadiliko ya Katiba


 Lulu akisindikizwa na askari Magereza.
Lulu akiingia katika gari la Magereza kwenda Rumande
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo.Picha Zote na Habari na Mdau Dande Francis
---
DAR ES SALAAM, Tanzania

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo ilimpatia masharti matano ya kupata dhamana kwa msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’,  anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.Masharti hayo yaliyolewa jana na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu, Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba mahakama hiyo impatie dhamana mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande tangu April mwaka jana ambapo walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha

148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .Jaji Mruke alisema ili mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe  kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi ,kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali  ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.Baada ya jaji huyo kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi uliokuwa ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza masharti hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo ofisini na hivyo kufanya Lulu kurudishwa rumande hadi leo atakapoletwa kwa ajili ya kujatimiza masharti hayo mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.Kufuatia mahakama hiyo jana kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi lake Na.125/2012 la kuomba mahakama hiyo impatie dhamana, lakini bado kesi ya msingi inayomkabili Lulu ambayo ni ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.Desemba 21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.


Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik Muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana usiku akitokea nchini Ethiopia ambapo alihudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za umoja wa Afrika(AU) uliofanyika jijini Addis Ababa.Picha na Freddy Maro-IKULU

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kata ya Pugu Kajiungeni Nuru Daniel akitoa shukrani zake za pekee kwa Serikali ya awamu na uongozi kwa kutekeleza ilani za Chama ikiwemo kuwapatia maji wakazi wa Pugu Kajiungeni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akisani kitabu cha wageni wakati wa Halfa fupi ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni. Kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela.
Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela akizungumza na wakazi wa Kata yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akitoa taarifa wakati akizindua Mradi wa Maji Pugu Kajiungeni ambapo amesema mradi huo unatokana na kisima cha maji chenye urefu wa mita 122 toka usawa wa ardhi.
Mstahiki meya amesema kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita 60,000 kwa saa. Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na mtandao wa mabomba wa kilometa 9, vituo 25 vya kuchota maji, nyumba ya pampu, fensi pamoja na uzio.
Aidha amewataka wananchi wa maeneo husika ya Pugu Kajiungeni ni kuitunza miradi hii na kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Pugu Emelda Samjela na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kassim Mjesa na Kulia ni Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd inayoshughulikia mradi huo Method Mlay.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wakazi wa Kata Pugu Kajiungeni watakaofaidika na mradi huo wakimsikiliza mstahiki Meya Jerry Silaa (hayupo pichani).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) barua rasmi ya mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni unaotekelezwa kwa ushirikiano na wahisani /wafadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Tanzania, Halmashauri ya manispaa ya Ilala na wafadhili wengine mbalimbali. Anyeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Kassim Mjesa.
Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) akitoa neno la shukrani baada Mstahiki Meya kumkabidhi barua rasmi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni na kuahidi kutoa ajira kwa Vijana wa maeneo ya Pugu kuanza sasa mpaka mradi utakapokamilika.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na wakazi wa Pugu baada ya kuzindua rasmi mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni ulioanza kubuniwa rasmi mwaka 2011.
Sehemu ya wakazi wa Pugu Kajiungeni waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo utakaochukua miezi Sita kukamilika na kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa sita kushoto) akikagua sehemu ya mradi huo kilipojengwa kisima chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita elf 60,000 kwa saa.
Muonekano wa Kisima hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa nne kushoto) na Diwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akingumza na vyombo vya habari ambapo amesema mradi huo wa maji wa Pugu Kajiungeni uhahudumiwa na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 140,000 lilipo katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto na matenki mnegine ya maji yenye ujazo wa lita 45,000 na 100,000 ambayo yanapatikana Pugu Kajiungeni karibu na Zahanati ya Pugu.
Amefafanua kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imechangia kiasi cha Shilingi 378,000,000 na kiasi kingine kinachobaki kinatolewa na Serikali Kuu pamoja na wahisani.
Mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi 1,024,000,000/=.