MWENYEKITI wa BAVICHA taifa ndugu John Heche ametoa wito na kuwaomba wanahabari kuchuja mambo ya kuandika yenye TIJA na maendeleo ya TAIFA tofauti na ilivyo sasa ambapo wanahabari wanaandika kitu chochote hata vingine visivyokuwa na msingi bali kujielekeza katika watu binafsi kujitafutia umaaarufu kupitia majina ya viongozi wakubwa ameyasema hayo akichambua hoja ya NAPE KUSEMA kuwa DR SLAA ANA KADI YA CCM, HECHE ameyasema hayo jana akiwa katika mazungumzo hapa eneo la KWEMBE ambako alikuwa na mualiko wa vijana jana alisema
KUHUSU HOJA YA KADI KUTOKUWA NA MASHIKO
.......

ndugu zangu unaposikia mtu anaanzisha maada ya katibu mkuu kuwa na kadi ya CCM hii inatusaidia nini sisi wananchi kutatua matatizo ya kukoswa maji?,elimu,huduma za afya , miundombinu, ardhi kuporwa,raslimali kuuzwa? hivi dr slaa akiwa na kadi ya CCM ndio maendeleo ya nchi yanazorota? au amewazuia ccm kutekeleza mambo ya msingi kwa sababu ya yeye kuwa na kadi ya ccm?
kadi ya CCM aliyokuwa nayo dr slaa alinunua au alichukua bure?
kama dr slaa angerudisha kadi hiyo ndio ingepata mtu mbadala na shupavu wa kuokoa nchi katika wale walio CCM ambaye sasa anakosa umakini kwa kukoswa kadi hiyo?

KATIBA ya chama( CCM) inasema ukijiunga na chama kingine unajifuta uanachama wa ccm auotomatically`mimi namshangaa Nape ndugu zangu ukiwa hauna akili kichwani ukipata uongozi haikusaidii kuongeza akili bali inakuanika zaidi jinsi usivyokua na upeo au ulivyomtupu, Dr slaa amegombea mara 3 ubunge kwa tiketi ya CHADEMA na amegombea urais na kuibiwa hapa alikuwa anagombea akiwa mwanaCCM?

AMUONYA NAPE ,,,,.....natoa wito rasmi na hili ntalitangaza kwenye vyombo vyote vya habari na kuwaeleza wananchi waelewe kuwa
NAPE hajawahi na haitatokea afikie level ya katibu mkuu wa CHADEMA kwa sababu
1 SIFA KUU iliyompatia Nape hata nafasi aliyonayo kwa sasa ni kulipwa FADHILA ya baba yake mzee Mosses Nnauye aliyekuwa Kampeini Meneja wa Kikwete kura za Maoni za CCM mwaka 1995

2 Nape huyu hajawahi hata kushinda cheo chochote cha kuchaguliwa na wananchi au hata na wana CCM wenzake
vyeo vyote alivyonavyo kapata kwa upenyo wa jina la baba yake huyu alikuwa mtoto wa mzee mosses ndio wale wale!sasa iweje ajifananishe au apate wapi uhalali wa kumjibu ama kumuattack DR! (SLAA!)sio kweli maana DR cv yake ni ya kushinda tena vyeo vya kugombe tunafahamu kuwa

Dr amekuwa mbunge miaka 15!jimbo la KARATU
Dr amekuwa makamu mwenyekiti wa chama
Dr amekuwa katibu mkuu wa chama
namtaka nape agombee hata uenyekiti wa mtaa ndio tuone kama atatoboa maana hata fomu ya wagombea nadhani hajui ilivyo asijifananishe na wanasiasa
mimi nadhani hawa watu wa kuteuliwa ama VYEO VYA KUBAMBIKWA WANAOSEMA OVYO KAMA CHIRIKU TUWAPUUZE KABISA NDUGU ZANGU
NASISITIZA PIA KUWA NAPE NI VUVUZELA KAMA ATAONA SI KWELI TUKUTANE NITAMUANIKA
alimaliza heche huku akishangiliwa na watu waliokuwepoClick image for larger version. 

Name: 2012-11-22 13.15.06.jpg 
Views: 0 
Size: 1.30 MB 
ID: 73644