JE TUNAJITAMBUA KAMA VIONGOZI AU WATAWALA? OLE WETU VIJANA WA TANZANIA....

HII NDIYO KANUNI YA KIONGOZI BORA, NA SIYO BORA KIONGOZI
K =KUBALI USHAURI
I=IELEWE HALI YA MAHALI ULIPO
0=ONDOA UPENDELEO NA UONEVU
N=NENA KAULI THABITI DAIMA

G=GAWA MADARAKA KWA UNAOWAONGOZA
O=ONYESHA MFANO KWA VITENDO
Z=ZUIA MIGOGORO MAHALA PA KAZI
I=IMARISHA KIWANGO CHA UTENDAJI

NASEMA OLE , OLE WENU MNAOTUMIA FURSA YA FEDHA,USHAWISHI WENYE GHILIBA NA MAHUBIRI YA UONGO ILI MJIPATIE UHALALI USONI PA UMMA NA KUIFANYA SIASA NI UTAWALA BAADALA YA UONGOZI.


HUU NI UJUMBE MAALUM KWA VIJANA WOTE  WAPENDA MADARAKA, KIMSINGI KINACHOTAFUTWA SI UTAWALA AU MADARAKA BALI NI UONGOZI TENA KWA MAANA HALISI YA UONGOZI NDANI YA JAMII YETU ILA KWA SABABU YA ULEVI WETU TENA WA KIJINGA WA KUPENDA UTAWALA,SIFA,HESHIMA NA MAMLAKA TUMEJIVIKA UPOFU NA SASA KWETU AGENDA NI UHESHIMIWA!!
KIONGOZI ANA MAONO, ANASHIRIKISHA JAMII MAONO YAKE,ANAYAISHI ILI JAMII IYAFUATE, KIONGOZI ANA AGENDA MTAMBUKA ITAKAYOTAFSIRI MIPANGO,MKAKATI NA MAJIBU YA JAMII YOTE KWA PAMOJA, KIONGOZI ANAAMINI KTK UMOJA,HAKI NA UPENDO. KIONGOZI NI YULE ALIYE TAYARI KUBEBA LAWAMA NA KUWA WA MWISHO KUPOKEA SIFA, NI YULE ANAYEAMINISHA,ANAYESIMAMIA ANAYOYAAMINI NA MATOKEO YAKE PIA. TUJIPIME KAMA TUNATAFSIRIKA HIVYO ROHONI MWETU, MIOYONI MWA JAMII NA NCHI AU TUNAUDANGANYA UMMA KWA UBINAFSI WETU?

NDUGU ZANGU, KABLA HATUJATANGAZA NIA, DHAMIRA NA WASIFU WETU NI VEMA SANA TUKARUDI KWA MWALIMU WA NCHI HII

"TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI, YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA FANAKA, MAJIRA YETU HAYA YANGEKUWAJE SASA?...UTUMWA WA NCHI NYERERE AMEUKOMESHA......"NINAKIRI KWA DHATI YA MOYO WANGU KUWA MIMI NI SHABIKI NA MUUMINI MWAMINIFU WA WIMBO HUU INAPOKUJA SIASA YA NCHI,JIMBO NA JAMII YANGU. 
KWA LEO NINAWOMBA MUITEMBELEE TAFSIRI HALISI YA UONGOZI NA TUONE KAMA TUNAPIMIKA KUELEKEA 2015.......LAKINI PIA KAMA KWELI KUNA HAJA YA KUKIMBILIA UONGOZI AU TUIACHE NATURE ICHUKUE MKONDO WAKE ILI HAKI NA DEMOKRASIA IJIPAMBANUE YENYEWE?
ASANTENI SANA; NORBERT A.NONGWA