MTO FURUWA, MTO FURUWA JAMANI....MH. DKT.MPONDA KANENA....

MTO FURUWA, MTO FURUWA, ONDOA MAFURIKO MALINYI KWA KUSHIRIKI KATIKA HARAKATI ZA KUUDHIBITI MTO FURUWA.

MH.MBUNGE DKT. HAJI MPONDA (0783-003635) ANAWAOMBA WANA MALINYI WOTE TULIO NJE YA MALINYI TUSHIRIKIANE NAYE KTK KUTAFUTA KIASI CHA TZSHS. 9.0MILIONI AMBAZO ZINAPASWA ZIWE MKONONI KABLA YA NOVEMBA 15,2012.

NIMEONGEA NA MH. MBUNGE ASUBUHI YA LEO, ANATUSIHI WANANCHI WENZAKE TUSHIRIKI KATIKA ZOEZI HILI KWA MANUFAA YA MJI WA MALINYI. YEYE KAMA MBUNGE AKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA ULANGA WAMEPATA CATERPILAR -D6 MAALUM KWA KAZI HII KWA GHARAMA HIYO YA MILIONI TISA. TUKILIKOSA KWA TAREHE HIZI TUNAPASWA KULIPIA MILIONI 15 BAADALA YA TISA. KWA TATHMINI YAKE ANAAMINI ZOEZI LITACHUKUA SIKU 3 TU KUKAMILIKA. NIMEOMBA WANA MDC/SACCOSS VIONGOZI TUKUTANE JPILI SAA SABA MCHANA ILI TUJUE WANA MALINYI DAR ES SALAAM NA HAPA JAMVINI TUNASIMAMA UPANDE UPI.

NDUGU, MALINYI NI URITHI WETU, NI MAMA NA BABA YETU, NI MAISHA YETU YA KILA SIKU JE NI NANI MWENYE JUKUMU LA KUISHI KWA NIABA YA MALINYI KAMA SI MIMI NA WEWE. NAOMBA USHAURI WENU, MAONI YENU NA MAARIFA YA KULITANZUA HILI TATIZO, MAONI YENU YATAPELEKWA MEZANI MDC KWA MAAMUZI NA UTEKELEZAJI.

NORBERT.A.NONGWA
malinyileoblogspot.com