ARDHI KWA KILIMO NI JANGA NA TISHIO JIPYA LA AMANI MALINYI

Wana Malinyi,UlaNGA-Kilombero napenda nitumie fursa hii kuwatahadharisha na hali tete inayokuja kwa jamii yetu kuhusiana na ardhi hususani mashamba.

Kwa hali ya sasa katika ukulima wetu kumejitokeza mageuzi makubwa sana kwa maana ya ukubwa wa mashamba yetu, aina mpya ya mazao ya biashara toka Pamba mpaka Mpunga.

Mengi yamejiri lakini sasa kuna kila dalili za dhuluma,uonevu, husuda na siasa chafu katika ardhi ya kilimo nyumbani Malinyi na pale Lupiro.

Malinyileoblogspot ameliweka jambo hili hadharani ili jamii ijitafakari, ijipange upya ili kuepuka madhara yajayo.

Karibuni kwa maoni wananchi.........