KIBOKO AMUUA MWANAMKE MVUVI

Bi Lucia Pangea (39-41) ameshambuliwa na kiboko wakati akiwa anavua samaki kwa mtindo wa kutanda na akina mama wenzake ktk mto Furuwa kwa Muhaku. Ni shambulio la ghafla kwa mama huyo na wenzake. Tukio hili limetokea jana jumanne na mazishi ya Bi Lucia Pangea yamefanyika leo huko Kipingo Malinyi Ulanga Morogoro. Mungu amrehemu Lucia Pangea na awape nguvu familia na umma wa Malinyi.